Waufukweni
JF-Expert Member
- May 16, 2024
- 5,383
- 18,776
Mbunge wa Jimbo la Mbogwe mkoani Geita, Nicodemas Maganga ameishauri Serikali kutumia njia aliyoiita ni rahisi ya kuwabaini watakatishaji fedha, ikiwa ni pamoja na pale anapoonekana mtu anafanya maendeleo lazima Serikali ijue imepata kodi kiasi gani.
Nicodemas amesema hayo bungeni Jijini Dodoma wakati akichangia bajeti ya Wizara ya Fedha kwa mwaka wa fedha 2025/2026 ambayo Bunge limeombwa kuiidhinisha.
"Fedha haramu zipo, unajuaje zipo?, unaweza ukamuona mtu anajenga ghorofa lakini hajulikani anafanya biashara gani, kwa hiyo kuna kila sababu anapoonekana mtu anafanya maendeleo fulani lazima tujue huyu anafanya biashara gani". amesema Mbunge Nicodemas