Mbunge wa Jimbo la Mbogwe mkoani Geita, Nicodemas Maganga, amesema ataendelea kuwa mkali na kusimamia kwa karibu matumizi ya fedha zinazotolewa na serikali kuu kwa ajili ya kutatua changamoto za wananchi na kuboresha miundombinu ya kijamii.
Mbunge Maganga ametoa kauli hiyo wakati wa mkutano wa hadhara uliofanyika katika Kata ya Ushirika, mkutano uliolenga kusikiliza kero za wananchi na kutoa taarifa ya utekelezaji wa miradi mbalimbali ya maendeleo chini ya serikali ya awamu ya sita.
Amesema ni wajibu wa viongozi na watendaji kuhakikisha kuwa fedha za serikali zinatumika kikamilifu kwa ajili ya kuboresha huduma za msingi kama elimu na afya, badala ya kuishia kwenye matumizi yasiyo na tija.