Mbunge Felista Deogratius Njau akichangia mada kuhusu Hotuba ya Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki amesema majengo kadhaa ya Ubalozi wa Tanzania yamechakaa likiwemo la Washington DC Nchini Marekani, hivyo ameshauri Serikali iangalie jinsi ya kuboresha.