Stephano Mgendanyi
JF-Expert Member
- May 16, 2020
- 2,833
- 1,301
MHE. NOAH LEMBRIS, Mbunge wa Jimbo la Arumeru Magharibi Akizungumza Kuhusu Bajeti ya Wizara ya Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalum Bungeni Jijini Dodoma
"Niliposoma taarifa ya Waziri wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalum, Mhe. Dkt. Dorothy Gwajima, katika maeneo yote sikuona sehemu yoyote na hata katika michango ya wabunge walipochangia ambayo taarifa ya Waziri imeonyesha Serikali au Wizara yake inashughulikia masuala ya Ushoga, Usagaji, na Ulawiti, Jinsi ambavyo Wizara inapambana au ina mikakati gani. Imeelezea kidogo sana na katika kujibu hoja mbalimbali hajaonyesha uzito wa michango ya wabunge kuanzia asubuhi kwa jinsi walivyochangia masuala ya ushoga, usagaji na ulawiti" - Mhe. Noah Lembris, Mbunge wa Jimbo la Arumeru Magharibi
"Taifa hili linatakiwa linusuliwe katika masuala ya Sodoma na Gomora. Tunataka kujua na kuona msimamo wa Serikali ituonyeshe dhahiri kuwa imechukia tatizo hili. Kama sitapata kauli nzito ya Waziri Dorothy Gwajima ya kusikitika, kupinga na kukemea ushoga na usagaji mimi sitaridhika" - Mhe. Noah Lembris, Mbunge wa Jimbo la Arumeru Magharibi