This is not correct in my humble opinion. Kama mtu hana facts hasa zinazohusu kuchafua au kupamba jina la mtu ni bora asiweke kabisa hapa. Inaweza kuwa tetesi, kwa hiyo nani athibitishe wakati anayetoa allegations ameshindwa kuthibitisha kutoka vyanzo vyake vya habari? Hii ikiachwa iendelee itafanya watu waje kwa malengo tofauti ya kuchafua au kuwapamba watu hapa, na hapo JF itapoteza credibility yake. Na kwa kuwa politics zina mambo mengi, hatuwezi kuthibitisha kama aliyeleta tetesi hapa si adui au rafiki wa mhusika anayesema. Impact ya mjadala wa hapa inaweza kuwa kubwa kwenye jamii, hasa kama facts na maturity hazizingatiwi katika mijadala inayoanza kama huu. Siwezi kuelewa lengo la mtu aliyeposti tetesi hii ni nini, inaonekana kuna agenda fulani, kama sivyo alete facts zinazothibitisha jambo hili, otherwise fact kwamba Ole Sendeka aliweza kusimama kidete kupinga ufisadi waziwazi Bungeni inasimama mpaka sasa, so give us the other side of Ole Sendeka and be brave to prove what u r saying!