Mbunge Oliver Semuguruka arahisisha usafiri kuwafikia wanaccm mkoa wa Kagera

Mbunge Oliver Semuguruka arahisisha usafiri kuwafikia wanaccm mkoa wa Kagera

Stephano Mgendanyi

JF-Expert Member
Joined
May 16, 2020
Posts
2,833
Reaction score
1,301
MBUNGE OLIVER SEMUGURUKA ARAHISISHA USAFIRI KUWAFIKIA WANACCM

Mbunge wa Viti Maalumu Mkoa wa Kagera CCM Mhe. Oliver Semunguruka ametoa Pikipiki 8 kwa Makatibu wa Jumuiya ya Umoja wa Wanawake Tanzania (UWT) kwa Wilaya zote za kichama mkoani Kagera.

Mhe. Oliver amesema kuwa amefikia hatua hiyo kutokana na changamoto walizokuwa wakipitia makatibu hao katika kuwafikia wanachama na kutekeleza Majukumu Yao.

Mhe. Oliver amesema kuwa Pikipiki hizo zimegharimu kiasi Cha shilingi Milioni 25.6 hadi kufika Bukoba na kufafanua kuwa yeye kama Mbunge amedhamiria kukisaidia Chama katika kuongeza wanachama na kuwasajli wakiwa majumbani kwao.

Kwa upande wa Mwenyekiti wa UWT Mkoa wa Kagera Hajat Faidha Kainamula amemshukuru Mbunge Oliver kwa jambo ambalo amelifanya na kusema kuwa kwa wakati wote amekuwa akitamani Wabunge waache alama katika Jumuiya yao huku mmoja wa makatibu ambao wamepokea Pikipiki hizo na kuzitumia akisema, Pikipiki hizo watazitumia kuhakikisha wanawafikia wanachama wengi.
WhatsApp Image 2023-02-26 at 13.55.08.jpeg
WhatsApp Image 2023-02-26 at 13.55.08(1).jpeg
WhatsApp Image 2023-02-26 at 13.55.08(2).jpeg
WhatsApp Image 2023-02-26 at 13.55.09.jpeg
 
Back
Top Bottom