Stephano Mgendanyi
JF-Expert Member
- May 16, 2020
- 2,833
- 1,301
MBUNGE OLIVER SEMUGURUKA: WANAWAKE CHUKUENI FOMU MGOMBEE SERIKALI ZA MITAA
Kuelekea uchaguzi wa Serikali za mitaa unaotarajia kufanyika mwezi Novemba mwaka huu, Mbunge wa Viti Maalumu Mkoa wa Kagera (CCM), Mhe. Oliver Semuguruka amewataka wanawake wilayani Ngara kujitokeza kuchukua fomu za kugombea nafasi hizo.
Mhe. Oliver Semuguruka ametoa wito huo wakati wa mkutano wa hadhara alioufanya katika mji mdogo wa Benako wilayani Ngara ambapo amesema kuwa kipindi hiki ni kipindi cha wakina mama kumuunga mkono Rais Samia kwa kugombea nafasi mbalimbali za uongozi.
"Wale watakaojitokeza kugombea atawaunga mkono na kuhakikisha wanashinda kwenye uchaguzi na kuwa kio cha jamii watakayoiongoza" - Mhe. Oliver Semuguruka, Mbunge wa Viti Maalumu Mkoa wa Kagera (CCM)
Aidha, Mhe. Oliver Semuguruka amewakumbusha wakina mama kuongeza bidii kwenye malezi ya watoto ambayo siku hadi siku maadili yao yamekuwa yakiporomoka na kusababisha kizazi cha sasa kukosa maadili katika jamii.