the guardian 17
JF-Expert Member
- Aug 15, 2024
- 395
- 570
Miaka mitano imeshaisha sasa miamba inaenda kuomba nafasi kwa miaka mitano mingine kisha wakapige makofi bungeni na kusisitiza kuwa vijana wajiajiri ilihali wao wamekomaliaga hapo tu.
===
Mbunge Mlugo ameaga rasmi katika Kikao cha Bodi ya Barabara kwa niaba ya wabunge wenzake, akihitisha kwa kutangaza kama Mwenyekiti wa Wabunge wa Mkoa wa Songwe kuwa kikao hicho ni cha mwisho kwao kabla ya uchaguzi mkuu ujao, Mlugo alieleza kuwa muda wa Bunge la sasa unakamilika kwa mujibu wa Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na wanaelekea kipindi cha uchaguzi 2025.
Katika kikao hicho, Mlugo pia alitangaza rasmi azma yake ya kugombea tena ubunge wa Wilaya ya Songwe kwa kipindi kingine, akieleza kuwa bado ana nia na dhamira ya kuwatumikia wananchi wa Wilaya ya Songwe
Soma: Pre GE2025 - Special Thread: Mijadala na Matukio ya Uchaguzi Mikoa yote Tanzania Bara na Zanzibar kuelekea Uchaguzi Mkuu 2025
Akiangazia maendeleo ya mkoa, Mlugo alitumia fursa hiyo kumpongeza Mkuu wa Mkoa wa Songwe,Daniel Chongolo, kwa uongozi wake thabiti na wa amani. Alieleza kuwa tangu Chongolo aingie madarakani, hakujawahi kutokea mgogoro uliosababisha viongozi wa kisiasa kama wabunge au madiwani kuwekwa ndani. Badala yake, changamoto zilizojitokeza zimeshughulikiwa kwa njia ya majadiliano, hali inayodhihirisha uongozi wa hekima na mshikamano.