Stephano Mgendanyi
JF-Expert Member
- May 16, 2020
- 2,833
- 1,301
Mbunge wa Viti Maalum Mkoa wa Iringa kupitia Umoja wa Wanawake Tanzania (UWT) Mhe. Rose Cprian Tweve amekuwa chachu ya maendeleo kwa wananchi wenzake kwa kujitolea kutoa matunzo na mahitaji yote muhimu kwenye kituo cha watoto cha Yerusalemu.
"Mimi kama Mwenyekiti wake Rose wa UWT Wilaya ya Mufindi nampongeza sana Rose kwa kazi kubwa anayoifanya kwenye kituo hiki, kwa kweli ni kazi kubwa anayoifanya kwenye jamii yake nyumbani kwake" - Mwenyekiti UWT Wilaya ya Mufindi
"Mhe. Rose ameweka watumishi watatu, anawalipa kila mwezi wanaofanya huduma ya kufua nguo za watoto, kuhakikisha watoto wanakuwa wasafi, wanakula vizuri; Mungu ambariki kwa kufanya mambo makubwa sana" - Mwenyekiti UWT Wilaya ya Mufindi
"Tunaendelea kumshukuru Mhe. Rose Tweve ambaye anaendelea kujitoa kwa michango yake na sadaka zake mbalimbali katika kituo hiki hasa katika kutusaidia kuwalea hawa watoto wa kituo hiki cha Yerusalem" - Dada na Mlezi wa Kituo cha watoto Yerusalemu
"Mungu ambariki na aendelee zaidi kumuongezea pale ambapo anapunguza.
Rose Tweve ameweza kutusaidia kusomesha watoto, Vyakula, Mavazi, Malazi na Magodoro. Bado anaendelea kusaidia ili kituo kiwe na usafiri wao wa gari kwenda shuleni wanaposoma" - Dada na Mlezi wa Kituo cha watoto Yerusalemu