Mbunge Saashisha Mafuwe asema kiwanda cha Kilimanjaro Machines Tools kinatengeneza aina zote za vifaa vya chuma, hakuna sababu ya kwenda China

Mbunge Saashisha Mafuwe asema kiwanda cha Kilimanjaro Machines Tools kinatengeneza aina zote za vifaa vya chuma, hakuna sababu ya kwenda China

Stephano Mgendanyi

JF-Expert Member
Joined
May 16, 2020
Posts
2,833
Reaction score
1,301
"Kiwanda cha Kilimanjaro Machines Tools karibu miaka 30 ni kama kilikuwa kimekufa. Nilienda Bungeni nikapiga kelele Serikali ikatuletea fedha, Mashine imejengwa imekamilika na Operation zinaendelea. Wateja wanaleta vifaa vya Makanika (Mechanics) vimeanza kutengenezwa hapa ndani ya Wilaya ya Hai" - Mhe. Saashisha Mafuwe, Mbunge wa Jimbo la Hai

"Nawaomba Watanzania wote wenye viwanda wanaohitaji uundwaji wa vyuma vya aina yoyote karibuni, iwe ni kutoka Migodi ya GGM, Barrick. Hauna sababu ya kwenda China. Tanga Mining wameleta kazi zao na wamekubali kazi nzuri" - Mhe. Saashisha Mafuwe, Mbunge wa Jimbo la Hai

"Ndani ya Kilimanjaro Machines Tools zinatengenezwa Mashine za kuranda Mbao, Mashine za Kusaga Mpunga, Trekta ambazo zinatengenezwa na Watanzania na zimethibishwa na TBS. Hakuna sababu za kwenda China kutafuta kifaa kwa miezi mitatu wakati kifaa kipo Kilimanjaro Machines Tools" - Mhe. Saashisha Mafuwe, Mbunge wa Jimbo la Hai.

 
Viwanda vya ndani vinazalisha sukari ya kutosha.

Mara ghafla vibali vikafutwa sukari ikaadimika.
 
Hongera muheshimiwa mbunge wa Hai
Tukilinde kiwanda Cha na hujuma za watu wa nje
 
Back
Top Bottom