Mbunge Sadifa alalamika, asema Wastara alimloga

Mbunge Sadifa alalamika, asema Wastara alimloga

Huyo

Hivi Mheshimiwa Mbunge anaamini kurogwa? Hii ndo 'Dinyalile Dinyale'. Ipo kaaaazi!
Yeye mwenyewe ni mtaalam wa ugagula.
Dakika chache kabla ya kutangazwa kuwa ndiyo mshindi wa nafasi ya mwenyekiti wa UVCCM alisikika akiongea na Simu akimuagiza mtu aliyeko zenji akimsisitisa afungulie majini yote kwani mambo sio mazuri nguvu zinamuishia.
 
Ya dunia mengi na yanahitaji uvumilivu guys,, Wastara needs courage, Mungu amsimamie
 
Uwezi ukawa kada mzuri wa CCM kisha ukawa mkweli.

Sadifa mwanaccm
Wastala mwanaccm.

Aaaahhh hiyo ndoa ya mume mrombo na mke mmachame
 
wastara ni pretender mkubwa sanaaa, kwa wasiomjua waweza kumuonea huruma na kuamini mambo yake lakini sio mtu huyo, alikuwa anamchukulia huyo bwana kama hawara na sio mme! alafu anapenda kuolewa kuliko mwanamke yetote hapo bongo movie! tulia ulee watoto wewe mama
 
Jamaa kaongea kimipasho sana! Hivi Mwanaume wa Kweli unawezaje kufunguka hivyo?
 
wastara ni pretender mkubwa sanaaa, kwa wasiomjua waweza kumuonea huruma na kuamini mambo yake lakini sio mtu huyo, alikuwa anamchukulia huyo bwana kama hawara na sio mme! alafu anapenda kuolewa kuliko mwanamke yetote hapo bongo movie! tulia ulee watoto wewe mama
Mambo Vipi cheupe dawa!
 
WASTARA-X-1.jpg

Aliyekuwa mume wa nyota wa Filamu za Bongo, Wastara Juma ambaye pia ni Mbunge wa Jimbo la Donge (CCM), Zanzibar, Sadifa Juma ameibua jambo zito miongoni mwa jamii akidai kuwa, mtalaka wake, Wastara Juma amekuwa akimroga.

Madai hayo aliyatoa Alhamisi iliyopita baada ya gazeti hili kumuuliza habari zilizoenea kwamba, amemuangukia Wastara akitaka warudiane kwani yaliyopita si ndwele.
Sadifa alisema kuwa, aligundua hilo la kurogwa baada ya Wastara kuondoka nyumbani kwake na kutangaza kwenye vyombo vya habari kuwa, amepewa talaka mbili.

Akizungumza kwa dakika 25, Sadifa alikwenda mbele zaidi kwa kusema: “Ukimwangalia Wastara harakaharaka unaweza kusema ni mwema sana lakini hana wema wowote. Hivi Wastara ni wa kuniroga mimi kweli?”
Alipoulizwa kuwa amepata wapi hizo habari za kulogwa Muheshimiwa akasema:

“Niliambiwa na watu wawili, mmoja dereva wangu, mwingine ni kijana wangu. Tena hao wameniambia juzi tu baada ya mambo kuharibika. Wakasema kuna siku walikwenda na Wastara kwa huyo mganga. Wastara alikuwa na ndugu yake mmoja.
Walipofika, vijana wangu hawakuingia. Kwa hiyo hawakujua walifuata nini! Mara ya pili akawaambia kuwa, wamekwenda pale kuchukua dawa eti ili isaidie ndoa yetu iwe na amani na mimi niache macho juujuu. Akapewa kombe kama unalijua kombe, aitie kwenye maji anipe ninywe."
“Sasa wale vijana wangu wakamshauri Wastara kwamba, kama maji hayo ya kombe atanipa yeye ninywe nikigundua itakuwa balaa, wakamwambia awape wao ndiyo wanipe mimi ninywe ili nikijua wataniambia ni dawa ya kukinga mwili. Lakini wao hawakunipa na wanayo mpaka leo (juzi, Alhamisi)!”

Akizungumzia suala la kupigia magoti Wastarra ili warudiane Sadifa alisema,
“Kwanza hizo habari si za kweli. Mimi wale mashemeji zangu waliniomba gari wamfuate ndugu yao. Nilitoa kwa ubinadamu tu, nikawawekea na mafuta.” na akadai kuwa mtu anayejitambulisha kuwa babu yake Wastarra sio babu yake ni bwana ake.

“Yule si babu yake Wastara. Yule ni bwana’ake kama hamjui. Mimi juzi tu ndiyo baadhi ya ndugu zake wameniambia ukweli kwamba yule babu, si babu yao bali alikuwa rafiki mkubwa wa marehemu Sajuki (Juma Kilowoko, aliyekuwa mume wa Wastara).”

“Sasa wewe jiulize, mkeo mnagombana, anakwenda kwa rafiki wa marehemu mume wake. Kwa nini asiende kwao? Kule anakaa kufanya nini? Yule Babu ndiye amenirithi mimi kwa Wastara.”

“Kuna wakati fulani Wastara aliumwa, dokta akamwambia atulie kwa muda asitembeetembee. Kesho yake akaniambia anakwenda Morogoro kwa huyo babu yake. Nilimkatalia, akalazimisha, akaenda. Sasa mke anawezaje kwenda mahali bila ridhaa ya mumewe?

“Alipokuwa kule, nikawa nampigia simu hapokei kwa muda wa siku tatu. Siku moja nyumbani alikuja kijana wake anayemfanyia biashara, nikamwambia Wastara yupo Morogoro, akampigia simu mbele yangu, akapokea, wakaongea. Walipomaliza, mimi nikampigia, hakupokea!”

SIKU YA WASTARA KUONDOKA NYUMBANI
“Mimi sikuwahi kutoa talaka kama Wastara anavyoeneza hizi habari. Siku hiyo anaondoka nyumbani mimi nilikwenda kwenye kamati za bunge, wakati naingia akanipigia simu na kusema anataka tuongee.

“Nilimwambia tutaongea baadaye yeye akataka muda uleule, nikakataa. Akasema anachotaka yeye nimpe shilingi milioni kumi afanye biashara. Nikamwambia sina, ndiyo akaondoka. Sasa jamani, mkeo kama anataka pesa ukamwambia huna ndiyo aondoke nyumbani? Mimi naona alifuata pesa tu.

Source: Gazeti letu pendwa
JIBU LA HAYO YOOOTE NI HILO ULILOSEMA MWENYEWE, HUYO ALIFUATA PESA
 
Hivi ikiwa hata habari za demu wangu hata mshikaji wangu siwezi kumwambia kama naona ni za mambo ya hovyo, sasa inakuwa kuwa vp watu waliokuwa kwenye ndoa wanaanza kuanikana hadharani bila kujali wayasemayo ni ya kweli au c kweli?! Sasa kesho na kesho kutwa mnarudiana wakati dume zima ushatangaza hadharani kwamba huyo unayemrejea anamegwa na mababu!!
 
Chezeya pesa wewe....utarogwa huku unajiona.Ila hawa watu wapole wapole, wanaopenda kujiliza liza huwa wana 'behind the scene' zao matata sana.
Umeongea ukweli mtupu huwa wana roho mbaya sana hao,wanaitwa silence killer
 
Back
Top Bottom