Stephano Mgendanyi
JF-Expert Member
- May 16, 2020
- 2,833
- 1,301
Wananchi zaidi ya 1000 wanaoishi katika kijiji cha Mavimba Kata ya Milola Wilayani Ulanga Mkoani Morogoro wamebaki bila makazi baada ya Mvua iliyoambatana na upepo mkali kubomoa Nyumba zaidi ya 100.
Wakizungumza na Waandishi wa habari waathirika wa tukio hilo wameiomba Serikali kupitia ofisi ya Mbunge wa Jimbo la Ulanga Salmu Almas Hashamu kuwasaidia misaada ya kibinadamu kwa kuwa baadhi yao wamekosa sehemu za kujihifadhi kutokana na nyumba zao kubomoka.
Soma Pia: Mvua zilizoambatana na upepo zaezua nyumba zaidi ya 100 Ulanga mkoani Morogoro
Diwani Kata ya Milola amesema kuwa upepo huu mkali ulitokea siku ya tarehe 31 Januari mwaka huu ambapo Mvua iliyoambatana na upepo iliharibu makazi ya watu na wengine kujeruhiwa.
Mbunge wa Jimbo la Ulanga, Salmu Almas Hasham akiambatana na viongozi wengine wamefika katika eneo hilo kuona jinsi ya kuwasaidia wananchi hao.
Salim amezitembelea nyumba zote ambazo zimekumbwa na janga hilo ambapo pamoja na mambo mengine ameahidi kutoa msaada kwa wakazi hao.