Waufukweni
JF-Expert Member
- May 16, 2024
- 5,383
- 18,776
Mbunge wa Misungwi mkoani Mwanza, Silvery Salvator amesema kuwa utekelezaji hafifu wa uamuzi na mijadala ya Bunge unakwamisha maendeleo na mafanikio ya Serikali.
Akichangia bajeti ya Ofisi ya Waziri Mkuu bungeni jijini Dodoma leo Jumanne, Aprili 14, 2026, Salvator ameeleza kuwa uzoefu wake binafsi unaonyesha changamoto kubwa katika upatikanaji wa huduma hata kwa viongozi.
“Nilienda mahali nikihitaji huduma ya kawaida ya kupewa barua, lakini licha ya wao kujua mimi ni mbunge mwenzao, ilichukua mwezi mzima kupatiwa. Taarifa hiyo nilimfikishia pia Profesa Shemdoe (Riziki Shemdoe),” amesema.
Ameongeza kuwa katika tukio jingine, alihitaji huduma ya kulipa kodi lakini hadi kufikia sasa miezi minne utekelezaji wake haupo. “Maana yake ni kwamba kama vitu tunavyoviongea humu haviwezi vikatekelezwa kwa vitendo, hatuwezi tukatoboa,” amesema.