Pre GE2025 Mbunge Samizi amuunga mkono Rais Samia kwa kugawa majiko ya gesi 400. Wananchi wamchukulia fomu

Pre GE2025 Mbunge Samizi amuunga mkono Rais Samia kwa kugawa majiko ya gesi 400. Wananchi wamchukulia fomu

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla, wakati na baada)

BWANKU M BWANKU

JF-Expert Member
Joined
Jan 12, 2019
Posts
377
Reaction score
435
IMG-20231227-WA0021.jpg

Mbunge wa Jimbo la Muhambwe mkoani Kigoma, Dkt. Florence George Samizi amesoma Utekelezaji wa Ilani ya Uchaguzi ya CCM kutoka mwaka 2020-2023 ambapo ametumia mkutano mkubwa uliofanyika katika ukumbi wa 10M Kibondo kueleza kwa wananchi wake mambo makubwa aliyoyafanya pamoja na Serikali ya Rais Samia Suluhu Hassan katika Jimbo lake hilo.

Kwenye mkutano huo, Dkt. Samizi amekabidhi majiko ya gesi 400 kwa wananchi wake, kutoa baiskeli 10 za walemavu pamoja na kugawa kadi za CCM 3,000 kwa wanachama.

Pia soma: Uzi Maalum wa Vibweka na Hekaheka za wanasiasa kuelekea Uchaguzi Mkuu 2025

Mbunge Samizi amesema Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan ameidhinisha Bilioni 52 kwa ajili ya miradi mbalimbali ya maendeleo inayoendelea kutekelezwa katika Jimbo lake la Muhambwe ambapo sasa kero za wananchi zinatatuliwa kwa kasi kubwa sana.


Mgeni rasmi kwenye shughuli hiyo kubwa alikuwa ni Katibu wa Halmashauri Kuu ya CCM Organaizesheni, Ndugu Issa Gavu.

"Rais Samia amedhamiria kumtua Mama kuni kichwani kwa miradi mingi ya maendeleo hapa Muhambwe. Miradi ya maji, miundombinu, elimu n.k. Ameidhinisha fedha zinazopeleka huduma kila mahali Jimboni kwetu Muhambwe." Alisema Samizi.

Kubwa zaidi Wana CCM wa Kata ya Rugongwe wametoa milioni moja ya kuchukua fomu ya Urais wa Dkt. Samia Suluhu Hassan muda utakapofika 2025, ikiwa ni ishara ya kumshukuru kwa kasi kubwa ya maendeleo inayofanyika kwenye maeneo yao.
 

Attachments

  • IMG-20231227-WA0017.jpg
    IMG-20231227-WA0017.jpg
    170.2 KB · Views: 9
  • IMG-20231227-WA0016.jpg
    IMG-20231227-WA0016.jpg
    87.6 KB · Views: 6
  • IMG-20231227-WA0007.jpg
    IMG-20231227-WA0007.jpg
    82.8 KB · Views: 6
Awe makini hizo kadi asije akawapa mamluki wa Act wazalendo maana chadema haipo maeneo hayo!
 
Back
Top Bottom