BWANKU M BWANKU
JF-Expert Member
- Jan 12, 2019
- 397
- 445
Mbunge wa Jimbo la Muhambwe mkoani Kigoma Mhe. Dkt. Florence Samizi hachoki wala kupumzika kulipambania Jimbo lake ambapo anafanya ziara kila kukicha na Bungeni anapambana kutafuta maendeleo ya Jimbo.
Baada ya kufanya ziara kubwa na nzito ya kuzungukia Jimbo na kusikiliza kero za wananchi na kuunga mkono shughuli zao za maendeleo, Mbunge Samizi amerudi Bungeni na leo Jumanne Aprili 29, 2025 ameuliza swali kuhusu Serikali kujenga Stendi ya Kisasa Muhambwe baada ya Halmashauri ya Kibondo kukamilisha andiko la ujenzi wake.
Akijibu swali la Mbunge Samizi kuhusu Ujenzi wa Stendi hiyo ya Kisasa Jimbo la Muhambwe, Naibu Waziri wa TAMISEMI Mhe. Dkt. Festo Dugange amesema "Niwapongeze Halmashauri ya Kibondo kwa kuandika andiko la ombi la ujenzi wa stendi ya kisasa, niwahakikishie wananchi Ofisi ya Rais- TAMISEMI kwa kushirikiana na Wizara ya Fedha inaangalia uwezekano wa kupata fedha kwa ajili ya ujenzi wa stendi hii na zingine kwa Halmashauri zenye uhitaji. Lakini ni maelekezo ya Serikali kwa Halmashauri kupitia mapato yao ya ndani watenge fedha kuanza ujenzi wa stendi hizi kwasababu ni mahitaji ya wananchi."