BWANKU M BWANKU
JF-Expert Member
- Jan 12, 2019
- 397
- 445
Atoa Bati 30 kwa Wajasiriamali na mifuko 30 ya saruji ujenzi zahanati Nyange
🗒️JUMATATU 21 APRIL 2025.
Mbunge wa Jimbo la Muhambwe Mhe. Dkt. Florence George Samizi, katika ziara yake leo Kata ya Mabamba ya kuwashukuru Viongozi wa CCM Kata, Tawi na Mashina kwa kushiriki vyema uchaguzi wa Serikali za Mitaa 2024. Na akiendelea kuwakumbusha namna ambayo Mkutano Mkuu wa CCM Taifa ulivyokwisha kumteua Mgombea kwa nafasi ya Urais na Makamu wake ambapo tayari Chama cha Mapinduzi Taifa kwa kauli Moja kilimteu Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan na Makamu wake Balozi Dkt. Emmanuel John Nchimbi, na kwa upande wa Zanzibar Mhe. Dkt. Ali Hussein Mwinyi.
Dkt. Samizi, amewaomba viongozi wa CCM Kata ya Mabamba kwa Umoja wao wahakikishe Dkt. Samia na Makamu wake Balozi Dkt. Emmanuel John Nchimbi, wanawapa kura za kishindo kwa kazi nzuri ambayo wamefanya ya kuleta fedha nyingi za kutekeleza miradi mbalimbali ya maendeleo katika Jimbo la Muhambwe akiwaeleza namna Serikali ya Dkt. Samia ilivyoleta mbilion 63 za Ujenzi wa Barabara ya lami Kibondo to Mabamba kuelekea nchi jirani ya Burundi, ambayo itachochea ukuaji wa kiuchumi ndani ya Kata ya Mabamba na Jimbo la Muhambwe kwa ujumla wake.
Aidha Mhe Samizi, ametoa Mabati 30 aliyoombwa na wajasiliamali wadogo wadogo katika Kijiji cha Nyange na kuwapa Simenti mifuko 30 kwa ajili ya kusapoti Ujenzi wa Wodi ya Mama na Mtoto Zahanati ya Nyange.
Kupata matukio na taarifa zote kwa kila mkoa kuelekea Uchaguzi Mkuu 2025 ingia hapa: Special Thread: Mijadala na Matukio ya Uchaguzi Mikoa yote Tanzania Bara na Zanzibar kuelekea Uchaguzi Mkuu 2025
Mbali na hayo Mhe.Samizi amepata nafasi ya kuwauliza viongozi wa CCM Kata, Matawi na Mashina kama wanaridhia ifikapo 28/6/2025 achukuwe fomu ya kuwania mhura wa pili wa kuwatumikia wananchi wake wa Jimbo la Muhambwe ambapo viongozi wote wa CCM Kata, Matawi na Mashina wamemhakikishia kumpa kura za kishindo na kumtaka asisubutu kuacha kuchukua fomu ya kuwania mhura wa pili.
Ikumbukwe Dkt. Samizi ni Mbunge anaekubalika kwa wananchi wake katika Jimbo la Muhambwe na mwenye ushawishi mkubwa toka aliposhika madaraka ya kuongoza wananchi wa Muhambwe, Samizi ni Mbunge ambaye ameonesha watangulizi wake hapa Muhambwe kuwa mwananchi ndie mwajili wa Mbunge na si vinginevyo.
#MUHAMBWE NA DKT. FLORENCE GEORGE SAMIZI-2025-2030#
Imetolewa Na:
Kitengo cha habari na mawasiliano Ofisi ya Mbunge wa Muhambwe.