Pre GE2025 Mbunge Samizi na kamati ya siasa yaendelea na ziara kata kwa kata

Pre GE2025 Mbunge Samizi na kamati ya siasa yaendelea na ziara kata kwa kata

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla, wakati na baada)

BWANKU M BWANKU

JF-Expert Member
Joined
Jan 12, 2019
Posts
377
Reaction score
435
Ziara ya Dkt. Florence George Samizi, Mbunge wa Jimbo la Muhambwe yazidi kupamba moto Jimboni akiongozana na Wajumbe wa Kamati ya Siasa ya Wilaya na Sekretaileti ya CCM Wilaya ya Kibondo chini ya Mwenyekiti wa CCM Wilaya Ndugu Hamis Salum Tahiro na Katibu wake Ndugu Rafael John Sumaye maarufu Control namba.

Ziara ambayo imejikita Mikutano ya ndani ya CCM yenye lengo la kuhamasisha viongozi wa matawi, kata, mabalozi pamoja na wajumbe wao, vitongoji, wenyeviti wa Vijiji namna ya kwenda nje kwa wananchi wakayazungumze mambo mazuri yaliyotekelezwa na yanayoendelea kutekelezwa na Serikali ya CCM chini Dkt Samia Suluhu Hassan.

Pia soma: Special Thread: Mijadala na Matukio ya Uchaguzi Mikoa yote Tanzania Bara na Zanzibar kuelekea Uchaguzi Mkuu 2025

Aidha katika ziara hiyo Mbunge Samizi ambae amefanya Mikutano 3 ya ndani Kata ya Busunzu akiwa na Mwenyeji wake Ndugu Paul Ngomagi Mavuko, Diwani wa Kata pamoja na Madiwani Viti maalum kimewatunuku vyeti vya pongezi Dkt. Florence George Samizi pamoja na Paul Ngomagi Mavuko Diwani wa Kata hiyo kwa kazi nzuri za kimaendeleo ambazo zimefanyika ndani ya Kata ya Busunzu ambapo Mwenyekiti wa CCM Kata ya Busunzu Ndugu Gilles Mpfunyigabho amewakabidhi vyeti hivyo.

Kamati ya Siasa na Mbunge Samizi kwenye ziara hiyo wamempongeza wagombea wa CCM Rais Samia, Dkt. Nchimbi na Rais Mwinyi kwa utekelezaji mzuri wa Ilani na kuwataka wanaccm kwenda nje kuelezea utekelezaji wa ilani kuimarisha Chama kuanzia ngazi ya shina.

IMG-20250303-WA0050.jpg


IMG-20250303-WA0052.jpg


IMG-20250303-WA0054.jpg
 

Attachments

  • IMG-20250303-WA0056.jpg
    IMG-20250303-WA0056.jpg
    580.8 KB · Views: 1
Back
Top Bottom