Stephano Mgendanyi
JF-Expert Member
- May 16, 2020
- 3,119
- 1,430
Mbunge wa Viti Maalum Mkoa wa Shinyanga, Mhe. Santiel Eric Kirumba Akichangia Bungeni Jijini Dodoma Hotuba ya Bajeti Kuu ya Serikali, Wizara ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora ameiomba Serikali kutupia jicho suala la upungufu wa Walimu Mashuleni na ongezeko la mishahara kwa Walimu ili kuongeza ufanisi katika kuinua viwango vya ufaulu kwa wanafunzi.
"Nampongeza Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa kuteuliwa kuwa Mgombea Urais kwenye uchaguzi ujao. Nampongeza Katibu Mkuu wa CCM, Mhe. Balozi Dkt. Emmanuel Nchimbi kwa kuteuliwa kuwa mtarajiwa wa Rais" - Mhe. Santiel Eric Kirumba, Mbunge wa Viti Maalum Mkoa wa Shinyanga
Kupata matukio na taarifa zote kwa kila mkoa kuelekea Uchaguzi Mkuu 2025 ingia hapa: Special Thread: Mijadala na Matukio ya Uchaguzi Mikoa yote Tanzania Bara na Zanzibar kuelekea Uchaguzi Mkuu 2025
"Miaka minne, Rais Samia Suluhu Hassan amefanya kazi kubwa kwenye Ofisi ya Utumishi wa Umma kwani amezingatia vigezo vya maadili, Kanuni na Sheria ambayo imewafanya watumishi wengi kupanda madaraja (vyeo) ambapo watumishi takribani 400,000 wamepandishwa madaraj. Pia ameongeza likizo ya uzazi kwa mwanamke ambaye amejifungua watoto njiti kwa wiki 40 na baba siku 7" - Santiel Eric Kirumba
"Rais Samia Suluhu Hassan ameongeza miaka ya utegemezi kutoka miaka 18 mpaka miaka 21 ambayo imeongeza NHIF wategemezi 65,000 ambapo sasa Serikali anatumia takribani shilingi bilioni 3 kuwahudumia. Serikali imejitahidi kutatua changamoto"
"Mwaka 2024 Rais Samia Suluhu Hassan alielekeza Watumishi Kada ya Walimu wapandishwe mishahara na madaraja. Serikali imejenga madarasa na kupeleka vitendea kazi. Lakini Waziri Simbachawene uje useme neno, umejipangaje kuwaongezea Walimu mishahara?"
"Maeneo ya Vijijini Serikali imeajiri Walimu lakini kuna shule zina upungufu wa Walimu. Mwalimu mmoja afundishe madarasa 3 ambaye inamlazimu watoto wafaulu na watoto wasipofaulu Serikali inatupia lawama shule husika. Muangalieni Mwalimu kwa kumuongezea Motisha la kumpandishia mshahara"
"Suala la ajira tuliweke kwenye Halmashauri, kila Halmashauri iwe na Kanzi Data (Database) ili iweze kutatua changamoto ya ajira. Mkoa wa Shinyanga tuna mradi wa SGR, Bomba la Mafuta, Umeme mkubwa wa Sola. Lakini wasomi wa maeneo ya miradi hawanufaiki na wananchi wenyeji hawashirikishwi"