PostGE2025 Mbunge Seif Suleiman aanza utekelezaji ahadi ujenzi Daraja Kwapeza

PostGE2025 Mbunge Seif Suleiman aanza utekelezaji ahadi ujenzi Daraja Kwapeza

Conversations and stories after Tanzania's 2025 General Elections

KwetuKwanza

Senior Member
Joined
Mar 13, 2023
Posts
127
Reaction score
245
169371.jpg


169374.jpg

5 January 2026

Jimbo la Ole limeandika ukurasa mpya wa maendeleo kufuatia kuanza rasmi kwa utekelezaji wa ujenzi wa Daraja la Kwapeza, mradi muhimu unaounganisha Shehia ya Ole na Vikunguni.

Utekelezaji huu ni matunda ya ahadi aliyoitoa Mwakilishi wa Jimbo la Ole, Mheshimiwa Seif Hamad Suleiman, kwa wananchi wake wakati wa ziara na mikutano ya hadhara.

Akizungumza katika muendelezo wa kuanza kwa ujenzi huo, Mheshimiwa Seif Hamad Suleiman amesema kuwa daraja hilo ni hitaji la msingi kwa wananchi wa maeneo hayo mawili, hasa katika kurahisisha usafiri, kuchochea shughuli za kiuchumi na kuimarisha mshikamano wa kijamii.

Ameeleza kuwa ahadi alizotoa ikiwemo ya leo kukabidhi mifuko 100 ya saruni kwa wananchi si maneno ya kisiasa bali ni dhamana ya uongozi yenye lengo la kuleta mabadiliko ya kweli.

“Daraja la Kwapeza si tu miundombinu ya kuvuka maji, bali ni daraja la matumaini, maendeleo na mustakabali bora wa wananchi wa Ole na Vikunguni,” amesema Mheshimiwa Seif.

Wananchi wa Shehia za Ole na Vikunguni wamepokea kwa furaha kubwa kuanza kwa mradi huo, wakieleza kuwa kwa muda mrefu wamekuwa wakikabiliwa na changamoto za kuvuka eneo hilo hasa nyakati za masika, jambo lililokuwa likihatarisha maisha na kuchelewesha shughuli za kijamii na kiuchumi.

Ujenzi wa daraja hilo utaondoa adha hiyo na kufungua fursa mpya za maendeleo, ikiwemo biashara, elimu na huduma za afya.

Viongozi wa shehia, wazee wa jadi na vijana waliokuwepo katika tukio hilo wamempongeza Mheshimiwa Seif Hamad Suleiman kwa kusimamia kwa vitendo utekelezaji wa ahadi zake, wakisema ni kielelezo cha uongozi unaowajali wananchi na unaothamini uwajibikaji.

Ujenzi wa Daraja la Kwapeza unatarajiwa kukamilika kwa mujibu wa ratiba iliyopangwa, huku mamlaka husika zikiahidi kusimamia ubora wa mradi huo ili uweze kudumu kwa muda mrefu na kuwanufaisha wananchi kwa vizazi vijavyo.

Kwa kuanza kwa mradi huu, Jimbo la Ole linaendelea kushuhudia utekelezaji wa miradi ya maendeleo inayolenga kuboresha maisha ya wananchi, jambo linaloonesha kwa vitendo falsafa ya uongozi wa kuahidi na kutekeleza.


Imetolewa na Ofisi ya Mwakilishi-Jimbo la Ole
 
Back
Top Bottom