Mbunge: Serikali haijawasilisha shilingi bilioni 1.5 za makato ya wafanyakazi kwenye Mifuko ya Hifadhi ya Jamii

Mbunge: Serikali haijawasilisha shilingi bilioni 1.5 za makato ya wafanyakazi kwenye Mifuko ya Hifadhi ya Jamii

Hii serikali ni ya kihuni na haipendi watu wake. Katika utawala wa J. Kikwete wastaafu walipata mafao yao katika kipindi kisichozidi miezi mitatu toka tarehe ya kustaafu.

Lakini tangu huyu muhuni aingie madarakani wastaafu wamekuwa wakisubiri mafao yao kwa mwaka mmoja na nusu hadi miaka miwili.

Fedha za mafao zinatumika kulipa mishahara ya wafanyakazi huku wastaafu wakipoteza maisha kabla hawajalipwa fedha zao.

Na anakwambia mniombee niendelee kutetea wanyonge na J2 huyo unamuona amepiga magoti akaishiriki meza ya bwana kwa unyenyekevuu kama anamaanisha vile,hahahahah
 
Hizo pesa wanazichukua bila idhini ya wenye nazo, wanazifanyia mambo yao kibabe, wanachelewa kuzirudisha, ndio maana leo unaambiwa kuna wastaafu wamefikisha miaka miwili bila kulipwa mafao yao, halafu wanajitapa "donor country"

Yani hawa jamaa hawana huruma kabisa na mtanzania, ni wakuogopwa sana, wanaleta siasa kwenye haki za wafanyakazi.

Ndio kiongozi wa wanyonge huyo.
 
"Kuna Bil 1.5 za makato ya wafanyakazi hazijawasilishwa, Serikali inachofanya inalipa mishahara lakini kwenye Mifuko ya Hifadhi za Jamii ile pesa haipelekwi, hii ni hatari mtu anapostaafu ili alipwe pesa zake anaambiwa michango yako huku haikuletwa" Mbunge ,Tunza Malapo.
View attachment 1460903

Chanzo: Darmpya Blog on twitter
Hali ya uchumi serikalini ni mbaya mno. Wanaficha tu lakini njaa haina mjanja
 

Attachments

  • chadema.jpg
    chadema.jpg
    13.9 KB · Views: 11
Kwanini unaongea kwa mahaba kwenye jambo serious?

Sent using Jamii Forums mobile app
Sio mahaba na siongei kishabiki. Kama kuna wastaafu zaidi ya kumi ninaowafahamu wamestaafu tangu mwezi wa April I, 2019 hadi Januari, 2020 na wote wamelipwa, nashindwa nini kusema hakuna ambaye hajalipwa? Kama hujalipwa au mzazi wako hajalipwa, nawe una haki ya kusema hawajalipwa.
 
Mimi ninawahanga wa kadhia hii labda kama kuna upendeleo unafanyika
Siwezi kukataa kwamba wengine hawajapata. Nakumbuka kuna wawili niliwasaidia hata kuandaa taarifa zao za awali za kustaafu kwaao mpaka tukajidhirisha kwamba taarifa zote zipo sahihi na kuhakikishiwa hivyo na mwajiri wao na PSSSF walipokuwa mwanachama. Baadab ya miezi kadhaa walipata mafao.

Ninachoweza kushauri ni kwamba wazee wetu wanahitaji maandalizi mazuri ya taarifa zao za kustaafu. Unawezakuta kuna nyaraka moja tu haipatikani kwa muda inasababisha mstaafu akae zaidi ya miaka miwili hajapata mafao yake. Hicho, kwa baadhi ya watu inaweza kuwa ni fursa ya kuwa na taasisi za kuwaandalia taarifa sahihi na timilifu wastaafu ili wasisumbuke mwishoni.
 
Mchungaji
"Kuna Bil 1.5 za makato ya wafanyakazi hazijawasilishwa, Serikali inachofanya inalipa mishahara lakini kwenye Mifuko ya Hifadhi za Jamii ile pesa haipelekwi, hii ni hatari mtu anapostaafu ili alipwe pesa zake anaambiwa michango yako huku haikuletwa" Mbunge ,Tunza Malapo.
View attachment 1460903

Chanzo: Darmpya Blog on twitter
Mchungaji fake wa river side ubungo analijua hili au jumapili ataamka na mbowe hivi kanisa lake halina pensioners ?
 
Back
Top Bottom