Mbunge: Serikali iwekeze kwenye miradi yenye tija

Mbunge: Serikali iwekeze kwenye miradi yenye tija

beth

JF-Expert Member
Joined
Aug 19, 2012
Posts
3,880
Reaction score
6,368
Tunza Malapo (Viti Maalum) amesema Mkoani Mtwara Soko la Chuno limejengwa kwa Bilioni 5.5 katika eneo ambalo ni tofauti na mwelekeo wa watu wengi akieleza, "Unaweza kujiuliza aliyependekeza Soko lijengwe kule alikuwa anawaza kitu gani? Maana yake ni Bilioni 5.5 zimelala pale hazina tija"

Aidha, Mbunge Kunti Majala naye amesema changamoto hiyo haina tofauti na ya Soko la Jiji la Dodoma ambalo limejengwa eneo la Nzuguni wakati Kata nyingi zipo upande wa Magharibi akisisitiza, "Wataalamu katika Miradi hii wanapoteza Kodi za Watanzania pasipo na tija"
 
Unaweza kukuta maamuzi ya kujenga hilo soko la Chuno yalifanyikia Dodoma au Dar es Salaam na hao wanaoitwa wataalamu. Hapo ndipo umuhimu wa ugatuzi wa madaraka unapokuja
 
Majina yenyewe
Tunza Malapo
Kunti Majala

Mleta mada umenifurahisha kwa kutotaja jina la soko la Dodoma..
 
Back
Top Bottom