Mbunge Shabiby ahoji utaratibu unaotumika kufungua nchi, atahadharisha Tanzania kugeuka shamba la bibi

Mbunge Shabiby ahoji utaratibu unaotumika kufungua nchi, atahadharisha Tanzania kugeuka shamba la bibi

Elitwege

JF-Expert Member
Joined
Jun 4, 2017
Posts
5,294
Reaction score
10,970
Mbunge aliyejawa na hoja zenye mashiko kwa taifa letu Mh Shabiby amehoji utaratibu unaotumiwa na serikali ya awamu ya 6 kufungua nchi kwani unaelekea kuigeuza Tanzania kuwa shamba la bibi kwa kila mgeni kufanya anavyotaka.

Bwana Shabiby amesema sasa hivi wageni hasa wachina wameruhusiwa kuingia nchini kiholela na kufanya biashara hata za kuuza karanga na viatu lakini watanzania hawaruhusiwi kuingia China hata kama umechanjwa chanjo ya kichina.

Shabiby amesema hiyo siyo diplomasia ya uchumi na huko siyo kufungua nchi mbali ni kuwafanya watanzania kuwa wachuuzi maisha yote ndani ya nchi yao.

 
Mzee wa praise team huyo ni mwana CCM mwenzio
Mimi sio praise team wala sio mwanaccm au chama chochote,mimi ni shabiki binafsi wa SSH, ila sitakagi ujinga..

Kuwa mwanaccm ndio nini? Kama anatetea biashara zake? Aweke ushahidi.
 
Kama Mchina anakuja Tanzania anafanya biashara ya karanga huku ana vibali halali na anapata faida then kuna mawili;

1. Fursa za biashara zipo nyingi Tanzania ila wananchi wetu hawazioni.

2. Tuwaige wachina kwa wanachikifanya mpaka wanapata faida.

Kinyume cha hapo tukiwa peke yetu hatuwezi kupiga hatua
 
Huyu ni mmojawapo ya Wabunge wanaoijua kazi yao Bungeni.
 
Back
Top Bottom