Mbunge aliyejawa na hoja zenye mashiko kwa taifa letu Mh Shabiby amehoji utaratibu unaotumiwa na serikali ya awamu ya 6 kufungua nchi kwani unaelekea kuigeuza Tanzania kuwa shamba la bibi kwa kila mgeni kufanya anavyotaka.
Bwana Shabiby amesema sasa hivi wageni hasa wachina wameruhusiwa kuingia nchini kiholela na kufanya biashara hata za kuuza karanga na viatu lakini watanzania hawaruhusiwi kuingia China hata kama umechanjwa chanjo ya kichina.
Shabiby amesema hiyo siyo diplomasia ya uchumi na huko siyo kufungua nchi mbali ni kuwafanya watanzania kuwa wachuuzi maisha yote ndani ya nchi yao.
Hoja yake ina mantiki ukiangalia jinsi Watz wanavohangaika na ajira sasa hivi. Forum aliyoongelea ni bungeni, wakitaka awapelekee ushahidi anaweza fanya hivo. Is absurd kudai ushahidi humu wakati mhusika haku adress hii forum.