Mbunge Shabiby: Kwanini Bandari Kavu ya Kwala haitumiki au kuna michezo ya rushwa inayoendelea nyuma ya Pazia?

Mbunge Shabiby: Kwanini Bandari Kavu ya Kwala haitumiki au kuna michezo ya rushwa inayoendelea nyuma ya Pazia?

Waufukweni

JF-Expert Member
Joined
May 16, 2024
Posts
5,383
Reaction score
18,776
Akichangia hoja Bungeni Aprili 9, 2026, Mbunge wa Jimbo la Gairo, Ahmed Shabiby, ametoa wito kwa Serikali kuitaka ianze kuitumia kikamilifu Bandari Kavu ya Kwala iliyopo mkoani Pwani ili kupunguza msongamano wa magari makubwa katika Jiji la Dar es Salaam.

Ameeleza kusikitishwa kwake na kitendo cha bandari hiyo kukaa bila kutumika kwa ufanisi wakati jiji likizidi kukabiliwa na foleni zinazosababishwa na maroli yanayobeba makontena.

Kuhusu uzinduzi: Rais Samia azindua Bandari Kavu ya Kwala Julai 31,2025

Shabiby amesema kuwa bandari hiyo ilijengwa kwa lengo mahususi la kutoa makontena yote jijini Dar es Salaam na kuyapeleka Kwala, ambapo kuna eneo kubwa lenye hekta nyingi linaloweza kuhifadhi makontena ya Meli hata 100 kwa wakati mmoja, bila kuleta adha mjini.

Katika mchango wake, Mbunge huyo amehoji kama kuna michezo ya rushwa inayoendelea nyuma ya pazia, akishangaa kwanini wafanyabiashara na wasafirishaji bado wanang’ang’ania kutumia bandari kavu (Dry Ports) zilizopo katikati ya mji kama vile Mwenge, Temeke, na Bunju.

Aongelee Jimbo lake la Gairo alilopewa mezani na chama chake.
 
Angekuwepo mwendazake ile bandari ya kwala ingekua inatumika na foleni Dar es salaam ingekua story, najiuliza Kama huyo mbunge kuna nini? Mbona haianzi kazi? Kwa akili zenu za mafuta lita pound 6000 na dola 800 mna cha kuwaambia wadanganyika?
 
Bandari kavu ya Kwala haijaanza kutumika kikamilifu kwasababu kipande cha SGR kutoka bandarini hadi hapo Kwala hakijakamolika. Kiko hatua za mwisho. Makontena na mizigo mingine itabebwa na SGR train hadi Kwala jambo ambalo halieezekani kwa sasa kwasababu kipande hiko hakijakamilika.

Ajabu kipande kifupi hivyo kinajengwa tangu 2021!
 
Ndio maana ana hoji kama kuna harufu ya rushwa.

Kumbuka hayo maeneo ya bandari kavu kati kati ya mji ni mali za watu wanapiga pesa.
 
Bandari kavu ya Kwala haijaanza kutumika kikamilifu kwasababu kipande cha SGR kutoka bandarini hadi hapo Kwala hakijakamolika. Kiko hatua za mwisho. Makontena na mizigo mingine itabebwa na SGR train hadi Kwala jambo ambalo halieezekani kwa sasa kwasababu kipande hiko hakijakamilika.

Ajabu kipande kifupi hivyo kinajengwa tangu 2021!

Hiko kipande cha SGR Hawajakipa Kipaumbele.
Kutoka Bandari hadi pale nadhan hakuzidi 80km.

Sasa toka 2021 Mwendazake alivyotutoka had leo Kipande hakijakamilika?. 🤔🤔🤔Inachukiza kwa kweli.

Na ni kweli, Magu angekuwepo hii bandar ingekuwa inafanya kazi.

Na Hata kikikamilika bado tutakaa miaka 4 tena mbele kusubiria Kichwa cha tren ya kubeba hayo makontena 😂😂😂

Folen ya magar kutoka Kurasin had Ubungo (km 15 tu hiv) unaweza kukaa masaa 3.
Na inasababishwa na Malori. Hasa ukikuta Lori moja tu limeharibika barabaran.

Mtaalam wa Magrafu 😂😂😂😂 hili hajashauriwa. Au nalo hana ujuzi nalo kwasababu yeye sio Fund.
 
Back
Top Bottom