upupu255
JF-Expert Member
- Sep 4, 2024
- 418
- 550
Mbunge wa Jimbo la Mtwara Vijijini, Shamsia Aziz Mtamba, amekabidhi msikiti kwa wahumini wa kiislamu wa Kata ya Ziwani, ikiwa ni hatua muhimu kwa maendeleo ya jamii ya Waislamu katika eneo hilo.
Ujenzi wa msikiti wa Jamiya ulianza miaka michache iliyopita, kwa juhudi kubwa za wahumini wa Kata ya Ziwani.
Licha ya kuwa na nia thabiti ya kumaliza ujenzi wa nyumba hiyo ya ibada, wahumini walikumbana na changamoto kubwa za kifedha.
Hali hii iliwalazimu wahumini hao kuungana na kumwandikia barua Mbunge wao, Shamsia Aziz Mtamba, wakimwomba msaada ili waweze kumaliza ujenzi wa msikiti huo.
Kupata taarifa na matukio yanayojiri kuelekea uchaguzi mkuu kwa kila mkoa ingia hapa: Special Thread: Mijadala na Matukio ya Uchaguzi Mikoa yote Tanzania Bara na Zanzibar kuelekea Uchaguzi Mkuu 2025
Wahumini walielezea kuwa ujenzi huu ni muhimu sana kwao, kwani ni sehemu ya ibada, elimu, na kukuza umoja wa kijamii katika kata hiyo.
Bila msaada kutoka kwa viongozi wao, walieleza kuwa ilikuwa vigumu kumaliza ujenzi na kuendelea na matumizi ya msikiti.
Kwa uapnde wake Mbunge Shamsia Aziz Mtamba amesema aliguswa na hali hiyo ya wahumini na alikubali ombi lao kwa haraka.
Aliwatembelea wahumini hao na kujionea changamoto walizokuwa wakikumbana nazo katika kumaliza ujenzi wa msikiti huo.
Alieleza kuwa aliguswa sana na juhudi za wahumini na aliona umuhimu wa kuwaidia ili kuhakikisha wanapata sehemu ya ibada ya kudumu.
Akizungumza wakati wa makabidhiano hayo, Mbunge Mtamba alisema, "Nina furaha kubwa kuona juhudi hizi za wahumini wa Kata ya Ziwani zikitimiza malengo yao ya kumiliki msikiti wao. Huu ni msaada wangu kwa jamii hii, na nitahakikisha kuwa kila mara nitakuwa bega kwa bega na wananchi wangu katika masuala ya maendeleo, hasa yale yanayohusiana na huduma za kijamii kama vile dini, elimu, na afya."