Stephano Mgendanyi
JF-Expert Member
- May 16, 2020
- 2,833
- 1,301
Mbunge wa Viti Maalum Mkoa wa Songwe, Mhe. Juliana Daniel Shonza amefanya Ziara ya Kata kwa Kata huku akipokelewa kwa shangwe na wananchi wa Kata ya Shiwinga iliyopo Wilaya ya Mbozi Mkoani Songwe.
Mhe. Juliana Daniel Shonza amesema kuwa lengo la ziara yake ni kuelezea Utekelezaji wa Ilani ya Uchaguzi ya CCM 2020-2025; Kuzungumza na Wanawake kuhusu utolewaji wa mikopo ya Asilimia Kumi (10%); Kuwezesha Wanawake Wajasiriamali Kiuchumi; Kuendesha Kampeni ya Kupinga Ukatili na Unyanyasaji wa Kijinsia; Kuendesha Kampeni ya Kupinga Mimba za Utotoni; Kampeni ya Kuhamasisha Lishe Bora kwa Mama na Mtoto.
Mhe. Shonza amesema kuwa kwa sasa Mkoa wa Songwe unaongoza kwa Mimba za Utotoni na Watoto kuacha Shule katika umri mdogo ambao wanapaswa kuwa Shule, hivyo Agenda ya Kupinga Mimba za Utotoni ni muhimu sana kutekelezwa.
Aidha, Mhe. Juliana Shonza ametoa fedha kwa Wanawake wajasiriamali wadogo wa Kata ya Shiwinga ikiwa ni lengo lake la kuwasaidia Wanawake kupata mitaji ya kuwainua kiuchumi katika shughuli za Kilimo ufugaji na biashara wanazozifanya
Vilevile, Mhe. Juliana Daniel Shonza amekabidhi Kadi za CCM na UWT kwa viongozi CCM na UWT wa Kata ya Shiwinga ikiwa ni muendelezo wa kuendelea kuvuna Wanachama Wapya ndani ya Chama Cha Mapinduzi na UWT ambao wamejiunga na CCM.
Mhe. Juliana Daniel Shonza amesisitiza sana Wananchi wote wa Kata ya Shiwinga kujitokeza kwa wingi Kujiandikisha katika Daftari la Kudumu la Mpiga Kura ili wapate haki ya kupiga kura wakati wa uchaguzi.
Mwisho, Mhe. Juliana Daniel Shonza amewasihi wananchi wote na viongozi kuendelea kumuunga mkono Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa kazi nzuri sana aliyofanya nchini ikiwemo Mkoa wa Songwe.