Mbunge: Simu zetu zinabeba taarifa nyeti na nzito, ataka Sheria itungwe kuzilinda. Ahoji ulazima wa 'Loss report'

Mbunge: Simu zetu zinabeba taarifa nyeti na nzito, ataka Sheria itungwe kuzilinda. Ahoji ulazima wa 'Loss report'

Replica

JF-Expert Member
Joined
Aug 28, 2017
Posts
1,681
Reaction score
8,887
Mbunge wa viti maalum, Judith Kapinga leo bungeni ameongelea kuhusu sheria ya ulinzi wa data na utaratibu wa kuomba 'Loss report'

LOSS REPORT
Mbunge Judith amesema utaratibu wa kuambiwa kutafuta 'Loss report' pindi mtu anapoteza laini ya simu. Mbunge amesema tulipofikia mtu anasajili laini ya simu kwa namba ya NIDA na anaweka alama za vidole hivyo utaratibu wa kutafuta loss report ni kuleta urasimu.

Ameendelea kwa kusema anahisi utaratibu umewekwa kwa ajili ya watu wa mjini, kijijini ili mtu afike kituo cha polisi kuomba 'Loss report' anatumia hela nyingi kwaajili ya loss report ya 500, hata kwenye simu mitandao inasumbua vijijini.

Mbunge ameomba utaratibu uondoke.

ULINZI WA TAARIFA BINAFSI
Judith amesema katiba ibara ya 16 inasema kila mtu anastahili kueheshimiwa ikiwemo kuheshimu mawasialiano yake binafsi.

Amesema simu zinabeba taarifa nyeti na nzito ambazo hata watu wa karibu hawafahamu. Pia simu zinabeba ulinzi wa fedha na maisha kwa ujumla hivyo kutokuwa na sheria ya ulinzi wa taarifa ni jambo linahatarisha.

Ameongeza yapo makampuni ya simu yanauza hizo taarifa mfano kwa kampuni za kubahatisha ndio maana watu wanapokea meseji hivyo kutumia taarifa za watu bila ridhaa ya wahusika.

Mwisho ametaka 'terms and conditions' ziwe kwenye lugha rafiki wakati watu wanasajili laini..
 
Back
Top Bottom