Mbunge Stephen Byabato awakutanisha Watoto yatima 200 Bukoba kwa Tamasha la Sadaka na Shukrani

Waufukweni

JF-Expert Member
Joined
May 16, 2024
Posts
2,060
Reaction score
5,648
Mbunge wa Jimbo la Bukoba Mjini, Wakili Stephen Byabato, kwa kushirikiana na wadau mbalimbali, wamewakutanisha watoto yatima 200 wanaoishi katika vituo vya watoto yatima Manispaa ya Bukoba.

Lengo kuu ni kuwapa faraja kwa kuwapa mahitaji muhimu ya shule, vyakula na mahitaji binafsi ikiwa ni sadaka na shukrani kwa Mwenyezi Mungu kutoka kwa wadau hawa kuelekea mwisho wa mwaka 2024.

Kundi la Songezi (WhatsApp Group) la Bukoba Mjini Mpya chini ya ulezi wa Mhe. Byabato na wadau nje ya kundi hilo ndio wamefanikisha tamasha hilo ambapo maandalizi yake ni zaidi ya Shillingi 10 Milioni zilitolewa na wadau na wamekabidhi sadaka mbalimbali kwa watoto yatima zikiambatana na tuzo za utambuzi kwa waanzilishi na vyeti vya shukrani kwa wasimamizi wa vituo hivyo kwa kazi kubwa ya kuijenga Jamii bora ya Bukoba.

Pamoja na zawadi nyingi zilizotolewa (zikiwemo za sikukuu), vimetolewa vitabu vya dini (Biblia na Quran Takatifu) yametolewa madawati 50 kwa shule za msingi zenye uhitaji zaidi za Byabato, Bilele, Rwamishenye na Bunena.

Aidha katika kuunga jitihada za Mbunge Byabato, Mdau kutoka Afrika Kusini, Injinia Datusi, ametoa vitanda 20 kwa watoto yatima, huku wafanyabiashara wa Soko Kuu Bukoba na wadau wengine wakitoa zawadi mbalimbali kwa watoto hao, TRA Kagera wakakamilisha furaha kwa kuwalisha wahudhuriaji wote zaidi ya 500 chakula cha pamoja.
 
When helping the poor, please leave camera at home. Usisaidie masikini kisha ukaanza kuwatangazia watu. Sasa huo ni msaada au masimango??
Nakubaliana na wewe asilimia zote mia moja,
Sisi wakristo kuna fungu kwenye biblia linasema ''Nilikuwa maskini mkaja kunitazama,nilikuwa kifungoni....''
sasa huwa najiuliza,kama tunaamini kwamba hao tunaowasaidia wanapokea kwa niaba ya Mungu, je naye tungempiga picha na kuweka kwenye mitandao?
 
It's totally and completely immoral mkuu. Ni kama vile mimi Alex nimekununulia wewe t-shirt kisha nikikuona umeivaa mbele ya rafiki yako wa kike kisha ninaanza kukuuliza, "mkuu, hii ndio ile t-shirt niliyokununulia juzi??

How would you my brother??
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…