Mbunge Subira Mgalu akagua miradi ya maendeleo Kerege, atoa maelekezo ya kutatua kero za wananchi

Mbunge Subira Mgalu akagua miradi ya maendeleo Kerege, atoa maelekezo ya kutatua kero za wananchi

Habari za Zanzibar

JF-Expert Member
Joined
Dec 18, 2024
Posts
651
Reaction score
433
MBUNGE SUBIRA MGALU AKAGUA MIRADI YA MAENDELEO KEREGE, ATOA MAELEKEZO YA KUTATUA KERO ZA WANANCHI

Mbunge wa Jimbo la Bagamoyo, Mhe. CPA Subira Khamis Mgalu, amefanya ziara ya kukagua miradi ya maendeleo na kufanya mikutano ya hadhara katika Kata ya Kerege, akisisitiza kuharakishwa kwa utekelezaji wa miradi ya afya, elimu, maji na miundombinu.

Akiwa katika mradi wa ujenzi wa Zahanati ya Kwa Kiwete, Mhe. Mgalu aliwahimiza wananchi na wadau kuendelea kushirikiana ili kuukamilisha mradi huo, huku akiahidi kuchangia mifuko 50 ya saruji na matofali 500. Amesema zahanati hiyo itapunguza msongamano wa wagonjwa katika Kituo cha Afya Kerege.

Katika Shule ya Msingi ya Serikali ya Mchepuo wa Kiingereza ya Genius iliyopo Matumbi, Mbunge huyo alimpongeza Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa kuanzisha shule hizo nchini na kuahidi kufuatilia changamoto zilizowasilishwa, ikiwemo upatikanaji wa majiko ya nishati safi kupitia taasisi husika.

Aidha, alitembelea Shule ya Sekondari Kerege kukagua maabara za kisasa kwa masomo ya sayansi katika shule hiyo na kuwataka walimu kuendelea kuimarisha malezi na maadili ya wanafunzi, huku akiwahimiza wanafunzi kujituma katika masomo, kuheshimu wazazi na walimu, na kuepuka kushiriki vitendo vya vurugu.

Katika mikutano ya hadhara iliyofanyika Nyakahamba na Kitonga, wananchi waliwasilisha changamoto za maji, barabara, maeneo ya kujenga huduma za kijamii pamoja na mikopo ya asilimia 10 ya Halmashauri.

Akijibu hoja za wananchi, Mhe. Mgalu alichangia Shilingi milioni 1.5 kwa ajili ya kuanza ukarabati wa Barabara ya Mapinduzi. Kuhusu malalamiko ya barabara iliyowekewa geti, alisema atakutana na viongozi na mamlaka husika kusikiliza namna suala hilo lilivyoshughulikiwa pamoja na hoja zilizotolewa na wananchi. Aidha, aliahidi kukutana na uongozi wa DAWASA kujadili suluhisho la kudumu la changamoto ya maji katika Kata za Kerege na Mapinga.

Mbunge Mgalu amesema ataendelea kufuatilia utekelezaji wa miradi ya maendeleo na kusimamia upatikanaji wa huduma bora kwa wananchi wa Jimbo la Bagamoyo.
 

Attachments

  • IMG-20260716-WA0067.jpg
    IMG-20260716-WA0067.jpg
    962.7 KB · Views: 12
  • IMG-20260716-WA0048.jpg
    IMG-20260716-WA0048.jpg
    899.9 KB · Views: 12
  • IMG-20260716-WA0042.jpg
    IMG-20260716-WA0042.jpg
    504.4 KB · Views: 14
  • IMG-20260716-WA0035.jpg
    IMG-20260716-WA0035.jpg
    1.1 MB · Views: 11
  • IMG-20260716-WA0065.jpg
    IMG-20260716-WA0065.jpg
    964.2 KB · Views: 11
  • IMG-20260716-WA0056.jpg
    IMG-20260716-WA0056.jpg
    625.8 KB · Views: 15
  • IMG-20260716-WA0058.jpg
    IMG-20260716-WA0058.jpg
    728.2 KB · Views: 11
  • IMG-20260716-WA0071.jpg
    IMG-20260716-WA0071.jpg
    935.6 KB · Views: 13
Back
Top Bottom