Stephano Mgendanyi
JF-Expert Member
- May 16, 2020
- 3,119
- 1,430
MBUNGE SUBIRA MGALU APONGEZWA NA UWT WILAYA YA BAGAMOYO KWA UTENDAJI MZURI
Chama wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Wilaya ya Bagamoyo Mkoani Pwani wamempongeza Mbunge wa Mkoa huo Bi, Subira Mgalu kwa kusema kuwa kiongozi huyo ni sawa na Lulu iliyotelemshwa na Mungu.
Wananchi walisema kuwa kwa jinsi ambavyo Mbunge Mgalu amekuwa akijitoa kwenye masuala mbalimbali ya kijamii pasipo kujali dini wala Kabila inaonyesha kabisa Bi, Mgalu ni kiongozi mwenye maadili mema na yenye hofu ya kesho yake.
Naye, Mwanahawa Hamja ambaye ni Mjumbe Kamati ya Utekelezaji UWT Wilaya ya Bagamoyo amempongeza Mhe Mgalu kwa kusaidia Jumuiya kwa kiwango cha hali ya juu katika masula mbalimbali ila kubwa ni la kutoa gari kwa lengo la kusaidia viongozi ili waweze kuwafikia wanachama wa ngazi za chini.
Kwa upande wake Katibu Mwenezi wa CCM Wilaya ya Bagamoyo Ramadhani Lukanga alisema kuwa Mhe Mgalu amekuwa nguzo imara sana katika kuhakikisha CCM inapata ushindi wa kishindo ndio maana ametoa gari kwa ajili ya kwenda kuwafikia wanachama kwa wepesi.
Aidha, amemtaka kuendelea kuwa na moyo huo wa kukisaidia Chama Cha Mapinduzi kwa lengo la kupata ushindi mnono kwa kura za Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt Samia Suluhu Hassan, Mbunge na Madiwani .
MWISHO
Attachments
-
Screenshot 2025-06-16 at 16-21-32 Nchi Kwanza (@nchikwanza) • Instagram photos and videos.png693.7 KB · Views: 36 -
Screenshot 2025-06-16 at 16-21-37 Nchi Kwanza (@nchikwanza) • Instagram photos and videos.png757.8 KB · Views: 39 -
Screenshot 2025-06-16 at 16-21-27 Nchi Kwanza (@nchikwanza) • Instagram photos and videos.png904.3 KB · Views: 32 -
1000553715qwasdert.jpg127.6 KB · Views: 29