Stephano Mgendanyi
JF-Expert Member
- May 16, 2020
- 2,833
- 1,301
MBUNGE SUBIRA MGALU: UWT CHINI YA MWENYEKITI WETU MAMA CHATANDA HATUJAAMINIWA KUJA KUUZA SURA, MRADI HUU UCHUNGUZWE
Jumuiya ya Umoja wa Wanawake Tanzania (UWT) ikiongozwa na Mwenyekiti wake Mama Mary Chatanda , imeviomba vyombo vya dola kuchunguza Mradi wa Ujenzi wa Shule ya Sekondari ya Ntomoko iliyopo kata Haubi mara baada ya kubainika kuwepo kwa dalili ya upigaji wa fedha za Mradi huo.
Hayo yamebainishwa leo tarehe 22 Novemba, 2023 na Mjumbe wa Kamati ya Utekelezaji UWT Taifa ambaye pia ni Mbunge wa Viti Maalum Mkoa wa Pwani na Katibu wa Wabunge Wanawake wanaotokana na Chama Cha Mapinduzi Ndugu. Subira Mgalu , alipotembelea na kukagua ujenzi wa shule hiyo ikiwa ni katika Ziara ya Mwenyekiti wa UWT Taifa Cde. Mary Chatanda alieambatana na Wajumbe wa Kamati ya Utekelezaji Taifa, WaNEC pamoja na Baraza Kuu.
Akikagua mradi huo, Cde. Subira amehoji ni sababu zipi ziliopelekea kutokuwa na Taarifa sahihi iliyoandikwa ya utekelezaji wa mradi huo ilikusudi na yeye kupata Nakala ya Taarifa hiyo kwa ajili ya mapitio badala yake imewasilishwa kwa kusomewa kwenye simu ya kiganjani
Aidha, Amehoji kwanini Taarifa hiyo haina mchanganuo wa matumizi ya fedha hizo za kiasi cha Milioni 544 na hata sababu zilizopelekea kucheleweshwa kwa ukamilishaji wa mradi huo hazikusemwa .
" _UWT Chini ya Mwenyekiti wetu Mama Mary Chatanda tuliaminiwa na Wanawake wote wa Nchi hii kwa lengo la Kumsaidia Rais wetu Mama yetu kipenzi Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan, na tunapokuja ziara hizi Viongozi wetu waliwasiliana nae na anatutuma kwa lengo la kumsaidia kazi sasa hatuwezi kuja tu hapa kuuza sura lazima tupate taarifa sahihi na tujionee kwa macho yetu kama kweli kazi inafanyika kama ilivyokusudiwa" - Mbunge Subira Mgalu
"Sasa katika hili niwaambie tu ukweli ni Halikubaliki, UWT kwa niaba ya Mwenyekiti wetu Mama Chatanda, tunaviomba vyombo vya dola kufanya uchunguzi katika mradi huu " Alisema Cde. Subira.
Mradi huo wa shule upo katika Kata ya Haubi Wilayani Kondoa na unagharimu fesha zaidi ya Tsh Milioni 544 ikiwa ni fedha kutoka Serikali Kuu.
Vilievile, mradi huo ulitarajiwa kumalizika mwezi wa Oktoba mwaka huu lakini hadi sasa bado haujamalizika.
#UWTImara
#UWTJeshiLaMamaSamia
#KaziIendelee
Attachments
-
WhatsApp Video 2023-11-23 at 15.53.14(1).mp442 MB
-
WhatsApp Image 2023-11-23 at 15.51.02.jpeg165 KB · Views: 6 -
WhatsApp Image 2023-11-23 at 15.51.03.jpeg147.3 KB · Views: 5 -
WhatsApp Image 2023-11-23 at 15.51.03(1).jpeg145.9 KB · Views: 5 -
WhatsApp Image 2023-11-23 at 15.51.03(2).jpeg141.3 KB · Views: 5 -
WhatsApp Image 2023-11-23 at 15.50.47.jpeg79.9 KB · Views: 5 -
WhatsApp Image 2023-11-23 at 15.50.46(3).jpeg73.3 KB · Views: 4 -
WhatsApp Image 2023-11-23 at 15.50.47(1).jpeg70 KB · Views: 5