Uchaguzi 2020 Mbunge Sugu ni mwanasiasa anayeweza kuisaidia nchi akitumika vizuri

Uchaguzi 2020 Mbunge Sugu ni mwanasiasa anayeweza kuisaidia nchi akitumika vizuri

Hapana, Sugu sio kilaza. Ni mwanasiasa wa kweli na mmoja wa vijana wanaotakiwa kuandikwa kwenye vitabu vya historia ya nchi yetu. Akiongeza elimu tu kidogo na kuwa na sifa rasmi za kitaaluma, basi anaweza kufaa kuwa top diplomat wa nchi yetu.

Mkuu kuwa kiongozi hapa Tanzania kuna hitaji hiyo elimu ya vyeti? Si ndio hayo hayo y kupata elimu ya darasani kwa kiingereza kisha mtu hata kuongea robo saa kwa kiingereza inakuwa kinyaa? Ili uandikwe kwenye vitabu vya historia ya nchi hii ni lazima uwe mwanaccm? Mbona una Ushawishi wa kitoto mno?
 
mtoa maada ovyo basi wote wapinzani wahamie ccm ili upinzani usiwepo ndo raya yenu.kama vip badilisheni katiba kiwe chama kimoja ujinga huu sasa

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mji wa mbeya si wakiasiasa yani wakazi wake wengi hawategemia siasa au mwana siasa ndio awaletee maendeleo, familia nyingi ziliona umuhimu wa shule mapema sana na ndio maana hata kabla ya shule za kata familia nyingi zilihakikisha mtoto anapomaliza elimu ya msingi kwenda sekondari ni lazima hivyo ikafanya vijana wengi kutoka familia nyingi wawe na shughuli zao za kuwapatia kipato ambacho kilienda badili maisha ya familia zao

Mbeya hakuna kundi la vijana wa buku saba yani wanategemea mbunge nani awabafilishie maisha yao vijana wengi wana shughuli zao

Mbeya wazee wengi ni wastaafu siyo wazee njaa njaa ambao wanataka upambe wengi wao walikuwa watumishi ambao maisha yao waliendesha kwa kipato cha shughuli zao si udananda furani

Wamama wengi mbeya wachacharikaji wana viapto vyao vya kupewa na watoto zao waliopo makazini au shughuli zao kwaiyo hawana njaa za khanga wala buku ten teni

Na ndio maana mneona mlinzi wa soko kawa meya sababu siasa sio shughuli za watu zinazowafanya waache mambo yao kama mikoa mingine

MY TAKE
Sugu atashinda tu sababu wana mbeya wanampenda hiyo ndio mbeya, upendwe sio ujipendekeze kingine mjue mbeya mjini ina ukabila ambapo mnyakyusa anapigwa vita kwaiyo ni vigumu sana mnyakyusa wakampa jimbo wasafwa, wakinga, nk hilo hawalitakagi kabisa
 
Asilimia zaidi ya 80 ya wabunge wa CCM ni mizigo!
 
Mtoa mada ni moja ya janga kwa taifa.Inaonesha ungekuwa mbunge wa upinzani na wewe ungenunuliwa zamani.Tambua kuwa Sugu anaweza kuhama chama na bado wanaMbeya tukamkataa.Ova

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Sugu ni mwanasiasa mzuri. Angekuwa na akili za mahesabu, angeshaukwaa uwaziri na kutumikia wananchi wa Mbeya kwa scope pana zaidi.

Ukweli mchungu ni hawezi kushindana na CCM kama imeamua 2020 asirudi bungeni. Siasa zimebadilika sana. Kama Magufuli na timu yake wameamua Mbeya irudi CCM, itarudi CCM.

Hata Maalim Seif aliamini atakuwa Rais wa Zanzibar 2015. Akajitangaza mshindi. Akavunja Katiba. Uchaguzi ukarudiwa, akasusa, akajua wananchi watafanya kitu. Hakuna lililofanyika. Akategemea Jumuiya za Kimataifa zitaingilia, yakatoka matamko mepesi tu. Sasa hivi kajiunga ACT anazeekea huko.

Sugu meza jeuri yako. Chagua upande unaoweza kukukuza kisiasa na kuwasaidia wananchi. Dunia ya sasa haijali harakati.
Kama wengine tu yuko pale kupata mkate kama walivyo ccm pia.
tapatalk_1582878491541.jpeg


Sent using Jamii Forums mobile app
 
Hapana, Sugu sio kilaza. Ni mwanasiasa wa kweli na mmoja wa vijana wanaotakiwa kuandikwa kwenye vitabu vya historia ya nchi yetu. Akiongeza elimu tu kidogo na kuwa na sifa rasmi za kitaaluma, basi anaweza kufaa kuwa top diplomat wa nchi yetu.
The MP Sugu is already one of top Diplomats,not like Kabundi & co.
 
Back
Top Bottom