Mbunge Suma Fyandomo ampongeza Dkt. Tulia kwa ushindi IPU

Stephano Mgendanyi

JF-Expert Member
Joined
May 16, 2020
Posts
2,833
Reaction score
1,301
Mbunge wa Viti Maalum Mkoa wa Mbeya, Mhe. Suma Fyandomo ametoa pongezi kwa ushindi mnono alioupata Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Tulia Ackson na kuwa Rais wa Umoja wa Mabunge Duniani (IPU)

"Pongezi za dhati kwa Spika wa Bunge letu, Mhe. Dkt. Tulia Ackson kwa kuchaguliwa kuwa Rais wa Umoja wa Mabunge Duniani (IPU). Ushindi huu ni ushuhuda wa kazi kubwa unayoendelea kuifanya na imani wajumbe waliyonayo juu yako na nchi yetu" - Mhe. Suma Fyandomo, Mbunge wa Viti Maalum Mkoa wa Mbeya

Itakumbukwa kuwa, Mhe. Spika Dkt. Tulia Ackson ameshinda kwa kishindo kuwa Rais wa Umoja wa Mabunge Duniani (IPU) kwa kupata kura 172 dhidi ya wagombea wengine kutoka Somalia ๐Ÿ‡ธ๐Ÿ‡ด (Kura 11), Senegal ๐Ÿ‡ธ๐Ÿ‡ณ (59) na Malawi ๐Ÿ‡ฒ๐Ÿ‡ผ (61).

Mhe. Suma Fyandomo amehitimisha salamu zake za Pongezi kwa kusema, "Mungu Ibariki Tanzania ๐Ÿ‡น๐Ÿ‡ฟ. Mungu Mbariki Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan. Mungu Mbariki Mhe. Dkt. Tulia Ackson.

 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn moreโ€ฆ