Mbunge Suma Fyandomo: Ukienda Mbeya Huoni Mji Uko Wapi

Mbunge Suma Fyandomo: Ukienda Mbeya Huoni Mji Uko Wapi

Stephano Mgendanyi

JF-Expert Member
Joined
May 16, 2020
Posts
2,833
Reaction score
1,301
Mbunge wa Viti Maalum Mkoa wa Mbeya, Mhe. Suma Fyandomo amesema kwa sasa mtu akifika katika Jiji la Mbeya hajui mjini ni wapi kutokana na mpangilio wa jiji hilo.

"Wananchi wa mkoa wa Mbeya, kiu yao wanatamani kuona jiji lile linafanana na majiji mengine," amesema Fyandomo akisema sasa hivi haijulikani mjini ni wapi.

Amesema hayo bungeni jijini Dodoma wakati akichangia bajeti ya Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi kwa mwaka wa fedha wa 2024/2025 na kuongeza kuwa changamoto kubwa inayowakabili ni ujenzi holela, na kwamba ikitatuliwa wakazi wa Mbeya watakuwa wameheshimishwa.

Ameongeza kuwa ni muhimu jiji hilo likawa lenye hadhi inayokubalika ikifahamika kwamba ndipo anapotoka Spika wa Bunge la Tanzania na Rais wa Mabungeni Duniani, Dkt. Tulia Ackson

Screenshot 2024-05-28 at 17-45-38 TBC Digital (@tbc_online) • Instagram photos and videos.png
 
Aiseee!Kwa hiyo pale ni mkusanyiko tu wa watu wanaolala na kuamka ili waendelee na mahangaiko ya dunia kabla ya kurudi tena kupumzisha vichwa vyao?
 
Back
Top Bottom