PreGE2025 Mbunge Tauhida Gallos atoa rai kwa Wananchi kushirikiana na Viongozi ili kuongeza ufanisi

PreGE2025 Mbunge Tauhida Gallos atoa rai kwa Wananchi kushirikiana na Viongozi ili kuongeza ufanisi

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla)

Stephano Mgendanyi

JF-Expert Member
Joined
May 16, 2020
Posts
3,119
Reaction score
1,430
Mbunge wa Viti Maalum Mkoa wa Magharibi kichama Mhe. Tauhida Gallos Nyimbo tarehe 24 Machi, 2025 akiwa katika Wilaya ya Magharibi B amewataka Wananchi kushirikiana na Viongozi wao ili waweze kufanya kazi kwa Ufanisi.

WhatsApp Image 2025-03-25 at 10.57.07.jpeg
Akizungumza katika ziara ya kuangalia Waasisi na Wagonjwa na kukabidhi Iftar, ikiwa ni kusherehekea miaka ya 4 Uongozi wa Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dk. Samia Suluh Hassan, Mbunge Tauhida Gallos amesema ushirikiano utasaidia Viongozi hao kuwaletea maendeleo Wananchi.

Mbunge Tauhida Gallos Amesema Waasisi na Wagonjwa wa UWT na Chama Cha Mapinduzi kwa ujumla, wamefanya kazi kwa Uzalendo na Uwajibikaji hivyo wanahitaji kuungwa mkono kwa hali na mali.

WhatsApp Image 2025-03-25 at 10.57.08.jpeg
Aidha, Mbunge Tauhida Gallos amewaomba Wananchi kuwaombaea Dua Viongozi wa Nchi ili wawe na Afya njema na kutekeleza majukumu yao kwa Ufanisi.

Kwa upande wake Mwenyekiti wa UWT Mkoa wa Magharibi kichama, Fatma Ali Ameir amesema ziara ya Mbunge Tauhida Gallos, imeongeza ari, motisha na hamasa kwa jamii.

WhatsApp Image 2025-03-25 at 10.57.09.jpeg
Hata hivyo, Fatma Ali Ameir amempongeza Mbunge Tauhida Gallos kwa kufanya ziara inayokwenda sambamba na miaka 4 ya Uongozi wa Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzanaia Mhe. Dk. Samia Suluhu Hassan.

Bi Safia Ali Khamis na Bi Asha Haji Abdallah ni miongozi mwa wagonjwa na Waasisi hao, wamesema wapata faraja kutokana na kupatiwa Iftari hiyo na kuomba Viongozi wengine kujitokeza kusaidia Wasiojiweza katika jamii.
 
Back
Top Bottom