Mbunge Tauhida Gallos na Ujenzi wa Nyumba za Makatibu UWT Mkoa wa Magharibi na Wilaya (Dimani na Mfenesini)

Mbunge Tauhida Gallos na Ujenzi wa Nyumba za Makatibu UWT Mkoa wa Magharibi na Wilaya (Dimani na Mfenesini)

Stephano Mgendanyi

JF-Expert Member
Joined
May 16, 2020
Posts
3,119
Reaction score
1,430

MBUNGE TAUHIDA GALLOS NA UJENZI WA NYUMBA ZA MAKATIBU UWT MKOA WA MAGHARIBI NA WILAYA ZAKE​

Mbunge wa Viti Maalum Mkoa wa Magharibi kichama, Mhe. Tauhida Cassian Gallos Nyimbo tarehe 11 Mei, 2025 alipokuwa akiwasilisha taarifa ya utekelezaji wa majukumu ya Mbunge amekabidhi fedha kwa ajili ya ujenzi wa nyumba ya Katibu wa UWT Mkoa wa Magharibi, Katibu wa UWT Wilaya ya Dimani na Katibu wa UWT Wilaya ya Mfenesini.

Akitoa ufafanuzi wa mchango wake, Tauhida Cassian Gallos Nyimbo amesema kuwa, Shilingi Milioni Tatu (3,000,000) ni ya ununuzi wa Matofali 2,500 kwaajili ya Ujenzi wa Nyumba ya Katibu UWT Mkoa wa Magharibi; Shilingi Milioni Moja (1,000,000) ni ya ununuzi wa Mifuko 50 ya Saruji kwaajili ya nyumba ya Katibu UWT Wilaya ya Dimani na Shilingi Milioni Moja (1,000,000) ni ya ununuzi wa Mifuko 50 ya Saruji kwaajili ya Ujenzi wa Nyumba ya Katibu UWT Wilaya ya Mfenesini.

Fedha hizo za michango, Tauhida Cassian Gallos Nyimbo amezikabidhi kwa viongozi wa UWT Mkoa wa Magharibi na viongozi wa UWT Wilaya ya Dimani na Wilaya ya Mfenesini huku akipongezwa na Katibu wa Kamati Maalum ya NEC, Idara ya Itikadi, Uenezi na Mafunzo CCM Zanzibar, Ndugu Khamis Mbetto Khamis.

Kwa upande wao, viongozi wa UWT Mkoa na Wilaya zote za Magharibi kichama wamemshukuru Tauhida Cassian Gallos Nyimbo kwa kipindi cha miaka mitano amekuwa akishughulika na changamoto za UWT na amewapa ushirikiano mkubwa kuzitatua na kumuomba aendelee kuwa na moyo huo huo wa uzalendo wa kuwatumikia wananchi.

Mwisho; Tauhida Cassian Gallos Nyimbo amewaomba wana UWT Mkoa wa Magharibi na Wilaya zake kuendelea kuwa na Umoja na kuhakikisha CCM inaendelea kushika dola hususani tunapoelekea kwenye uchaguzi mkuu Oktoba 2025.
 

Attachments

  • WhatsApp Image 2025-05-12 at 09.05.35.jpeg
    WhatsApp Image 2025-05-12 at 09.05.35.jpeg
    97.2 KB · Views: 30
  • WhatsApp Image 2025-05-12 at 09.05.37.jpeg
    WhatsApp Image 2025-05-12 at 09.05.37.jpeg
    76.6 KB · Views: 33
  • WhatsApp Image 2025-05-12 at 09.05.35 (1).jpeg
    WhatsApp Image 2025-05-12 at 09.05.35 (1).jpeg
    99.1 KB · Views: 36
  • WhatsApp Image 2025-05-12 at 09.05.42.jpeg
    WhatsApp Image 2025-05-12 at 09.05.42.jpeg
    99.1 KB · Views: 31
  • WhatsApp Image 2025-05-12 at 09.05.41.jpeg
    WhatsApp Image 2025-05-12 at 09.05.41.jpeg
    105.1 KB · Views: 34
  • WhatsApp Image 2025-05-12 at 09.05.40.jpeg
    WhatsApp Image 2025-05-12 at 09.05.40.jpeg
    107.7 KB · Views: 31
Back
Top Bottom