Mbunge Tauhidi viti maalumu CCM Kalidanganya Bunge Elimu yake ya DIPLOMA , this is Serious !!


yaani hata yeye ukimuuiza alisoma wapi na lini?? hawez kukupa majibu sahihi

afande murilo kamata huyo mbunge tapeli, anagushi mihuri ya taasisi
 
Huyu akipewa Mtihani wa Civics wa form 2 ili kupima ufahamu wake wa elimu ya uraia inaweza ikawa ni shughuli pevu🐼
 
Nilinde kisiasa na nami nikulinde kwenye biashara zako

Nikosoe kwenye siasa nami nikuletee vikwazo kwenye biashara zako.

Chagu Moja ,
 
Na Bashite mbona anadunda tu pamoja na wizi wa cheti! Ni wengi tu nchi hii kwenye ngzi za juu.
 
Sumaye alisema ukitaka biashara zako ziendelee peperusha bendera ya CCM.
 
Huyu kadanganya Bunge , nmekutafuta hiki chuo usiku kucha, sijakupata na hakipo popote pale Duniani
 
Ukiprkua namna hiyo pale Mbungeni utabaki na wabunge wasiozidi 30!!
 
Huyu mama kwa zile pumba ingekuwa ndio mke wangu nilikuwa nampa taraka tastu.

Huwezi kuishi na kiumbe asiyejali utu kiasi kile kwasababu ya madaraka.
 
Hivi ana uraia pacha?
 
Dah, kumbe ndo maana i see!
Sekondari miaka 15, na bado kuna diploma kapata wakati anamalizia elimu ya sekondari
Tumia akili na pendekezo lake la wabunge kuwa na Masters likifanyiwa kazi, nchi yetu itapona.
 
Tanzania sasa inakumbwa na kashfa nyingine kubwa inayogusa uadilifu wa viongozi, baada ya mashaka makubwa kutanda kuhusu elimu ya mmoja wa wanasiasa vijana waliojitokeza kwa sauti kubwa kisiasa katika miaka ya karibuni. Taarifa mpya zimeibua tuhuma nzito kuhusu cheti cha diploma anachodai kukipata kati ya mwaka 2013 hadi 2015, ambapo nyaraka zake zimeonekana kujaa mapungufu ya kushangaza na yasiyoelezeka kitaaluma.

Katika cheti kinachozungumziwa, chuo kilichoandikwa ni Community Concern Trainung Institute, jina ambalo hata kwa muonekano wake linaonyesha makosa ya tahajia kwa kuandika "Trainung" badala ya "Training". Mbali na kosa la tahajia, uchunguzi wa haraka umebaini kuwa hakuna chuo chenye jina hilo kilichosajiliwa nchini Tanzania, wala hakipo katika orodha ya vyuo vinavyotambuliwa na Baraza la Taifa la Elimu ya Ufundi na Mafunzo ya Ufundi Stadi (NACTE).

Hii imepelekea wengi kujiuliza, ni vipi mtu aliyeshindwa mara kadhaa mitihani ya kidato cha nne na sita, na aliyekuwa akisoma kwa tabu katika Sekondari ya Ubago kati ya 2013 na 2015, angeweza kwa wakati huo huo kusoma na kupata diploma kutoka chuo kisichojulikana? Hii inaacha maswali magumu ambayo yanahitaji majibu ya dharura, si kwa maneno, bali kwa nyaraka na ushahidi thabiti.

Aidha, hoja kwamba chuo hicho huenda kiko nje ya nchi nazo zimepokewa kwa mashaka makubwa, kwani hakuna kumbukumbu zozote zinazoonyesha kuwa mtu huyo alisafiri nje ya nchi kwa ajili ya masomo katika kipindi hicho. Badala yake, ushahidi wa mitihani aliyokuwa akiifanya nchini Tanzania katika kipindi hicho unakinzana kabisa na madai yake.

Hali hii imezidi kuibua hofu miongoni mwa wananchi na wadau wa elimu kuwa huenda kuna viongozi kadhaa wenye nyaraka bandia au zisizo na uhalali wowote wa kitaaluma, lakini wamefanikiwa kupenya katika nafasi za juu kwa misingi ya hila na si vigezo halali.

Wito umetolewa kwa mamlaka husika kama TCU, NACTVET na TAKUKURU kufanya uchunguzi wa kina kuhusu sifa za elimu za watu wanaoshika nafasi za umma, ili kujenga mfumo unaozingatia ukweli, uwazi, na uadilifu.

Ikiwa kweli tuna ndoto ya taifa lenye haki, basi hatuwezi kuruhusu viongozi waongo kuendesha nchi kwa kutumia vyeti vya kubumba. Je, jamii iko tayari kudai uwajibikaji wa kweli? Au tunaendelea kufumba macho hadi tusonge ukingoni?
 
Secondary school kasoma miaka 15, shule ya msingi miaka 8.
Bunge likivunjwa mwezi ujao anapata milioni 400 za Watanganyika.
 
Je, ni Mbunge mwingine 'kihiyo.'?
 
yaani hata yeye ukimuuiza alisoma wapi na lini?? hawez kukupa majibu sahihi

afande murilo kamata huyo mbunge tapeli, anagushi mihuri ya taasisi
Polisiccm IGP Bishungwa lao ni moja wote wamekumbatia vitendo haramu vya kishetani
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…