PreGE2025 Mbunge Toufiq Turky Agawa Misaada ya Sikukuu kwa Wananchi wa Makundi Maalum

PreGE2025 Mbunge Toufiq Turky Agawa Misaada ya Sikukuu kwa Wananchi wa Makundi Maalum

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla)

Stephano Mgendanyi

JF-Expert Member
Joined
May 16, 2020
Posts
3,119
Reaction score
1,430

MBUNGE TOUFIQ TURKY AGAWA MISAADA YA SIKUKUU KWA WANANCHI WA MAKUNDI MAALUM​

Mbunge wa Jimbo la Mpendae, Mhe. Toufiq Salim Turky tarehe 06 Juni, 2025 ametembelea Shule ya Sekondari ya Mpendae na kukabidhi Misaada ya Sikukuu kwa makundi mbalimbali ya watu wenye mahitaji Maalum wakiwemo Mayatima, Walemavu, Wajane, Wazee.

Mhe. Toufiq Salim Turky aliambatana na Mhe. Ussi Pondeza, Mbunge wa Jimbo la Chumbuni; Mwakilishi wa Jimbo la Mpendae, Mhe. Shaaban Ali Othman; Katibu wa Kamati Maalum ya NEC, Idara ya Itikadi, Uenezi na Mafunzo, Mhe. Mbetto Khamis Mbetto; pamoja na Madiwani wa Wadi za Jimbo la Mpendae.

Aidha, Mhe. Toufiq Salim Turky amesema kuwa, ametoa Sadaka ya Sikukuu kwa Wazee, Watu wenye Ulemavu na wanaoishi katika mazingira magumu ikiwa na lengo la kuwasaidia na kuwapa faraja hususan kipindi hiki cha Sikukuu.

Akizungumza katika mkutano na wananchi hao, Toufiq Salim Turky ameowaomba na kuwasisitiza viongozi hao wa Jimbo la Mpendae, wamesisitiza kuendelea kuisaidia jamii yenye uhitaji ili nao washereheke Sikukuu kwa furaha na upendo.

Mwisho, Misaada hiyo imetolewa kwa zaidi ya wananchi Elfu Moja (1,000) wa Jimbo la Mpendae ambao wamenufaika na Sadaka hiyo ambapo wamewashukuru sana viongozi kwa kuwatembelea na kuwakumbuka.

WhatsApp Image 2025-06-09 at 15.16.50 (1).jpeg
WhatsApp Image 2025-06-09 at 15.16.55.jpeg
WhatsApp Image 2025-06-09 at 15.16.54.jpeg
WhatsApp Image 2025-06-09 at 15.16.50.jpeg
WhatsApp Image 2025-06-09 at 15.16.49 (1).jpeg
WhatsApp Image 2025-06-09 at 15.16.49.jpeg
 
hawa jamaa wanadhalilisha watu sana, yani unampa mtu sadaka na picha kibao unampiga. watu wanashindwa hata kujali heshima zao kwa kuendekeza njaa
 
Back
Top Bottom