PreGE2025 Mbunge Toufiq Turky: Ukiwa yatima au mjane Jimbo la Mpendae unalipwa posho

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla)

Stephano Mgendanyi

JF-Expert Member
Joined
May 16, 2020
Posts
3,119
Reaction score
1,430

MBUNGE TOUFIQ TURKY: UKIWA YATIMA AU MJANE JIMBO LA MPENDAE UNALIPWA POSHO​

Mbunge wa Jimbo la Mpendae Toufiq Turky amesema bado ana nia ya kuendelea kuwa mbunge wa Jimbo hilo kutokana na utekelezaji mkubwa wa Ilani ya Chama cha Mapinduzi Jimboni kwake.

Turky amesema hayo leo Jijini Dodoma alipokuwa kushiriki Mkutano Mkuu Maalum wa chama hicho ambapo ameeleza kuwa katika jimbo lake hakuna changamoto kabisa ya maji, huku ujenzi wa barabara kwa kiwango cha lami ukiwa umefanyika kwa kiwango kikubwa pamoja na uwepo wa shule za Kisasa ambazo zimejengwa katika hadhi ya ghorofa kuanzia chekechea mpaka kidato cha sita.

Turky ameongeza kuwa katika kujali wananchiwa Jimbo hilo yeye mwenyewe huwa anawalipa mshahara viongozi wa dini pamoja na kutoa fedha za kujikimu kwa mayatima. Huku akiweka kiyoyozi(AC) katika nyumba zote za Ibada(misikiti na makanisa).

Turky amesema Kwa upande wa vijana yeye binafsi ametoa ajira zisizo pungua 800 kwa vijana wa jimboni kwake.

Kura zinatafutwa hata kwa kampeni zisizo za kweli
 
Back
Top Bottom