Stephano Mgendanyi
JF-Expert Member
- May 16, 2020
- 3,119
- 1,430
MBUNGE MWANAISHA ULENGE AITAKA SERIKALI KUKIWEZESHA KITUO ATAMIZI CHA MKONGE TANGA
Mbunge wa Viti Maalum, Mhandisi Mwanaisha Ulenge amesisitiza umuhimu wa Serikali kuhakikisha fedha zilizotengwa kufanikisha mradi wa kituo atamizi cha uzalishaji wa bidhaa za mkonge kinachowahusisha vijana, wanawake na watu wenye ulemavu zinafika kwa wakati kwa walengwa.
Akizunguma bungeni kwenye mjadala wa bajeti ya Wizara ya Kilimo, Mhandisi Ulenge amesema tayari Serikali imetenga shilingi milioni 600 kwa ajili ya kuendeleza shughuli za kituo hicho.
Mbunge huyo amehimiza bidhaa hizo kuzalishwa kwa wingi ili zitumike ndani ya nchi na pia katika masoko ya kimataifa, hatua itakayosaidia kuongeza thamani ya zao la mkonge na kuinua uchumi wa vikundi vinavyohusika na mradi huo.