The Watchman
JF-Expert Member
- Nov 7, 2023
- 2,186
- 4,940
Mbunge wa Viti maalum Mkoa wa Kilimanjaro Esther Maleko amesema serikali ya awamu ya sita ya Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan imetoa zaidi ya Bilion nne (4) katika Halmashauri ya Wilaya na ameunga mkono jitihada zinazofanywa na Serikali kwa kutembelea Hospitali ya Wilaya Hai na Kugawa Shuka zaidi ya Hamsini (50)
Hospitali ya Wilaya pekee imepokea Milioni 900 kwa ajili ya Ujenzi wa Njia za Kutembelea (Walk Way) Zaidi ya Kilomita 1, Ujenzi wa Bohari ya Dawa, Ujenzi wa Maabara ya Kisasa, Wodi ya Kujifungulia (Matenity Ward), na Private Ward. Aidha Serikali imetoa Milioni 250 Ujenzi wa Wodi ya ICU na Milioni 300 ununuzi wa Vifaa vya ICU pamoja na zaidi ya Milioni 196 Ununuzi wa X - Ray Mashine.