Stephano Mgendanyi
JF-Expert Member
- May 16, 2020
- 2,833
- 1,301
MBUNGE VUMA HOLLE AENDELEA KUZISAKA KURA KWENYE MVUA
Mbunge wa Jimbo la Kasulu Vijijini, Mhe. Augustine Vuma Holle ameendelea na Kampeni za kuwaombea kura wagombea wanaotokana na CCM katika uchaguzi wa Serikali za Mitaa Unaotarajiwa Kufanyika tarehe 27 Novemba, 2024 wakati Mvua ikiendelea kunyesha.
Katika Kampeni zake, Mhe. Augustine Vuma amesema kuwa wakati Chama Cha Mapinduzi (CCM) kinajiandaa na suala la uchaguzi wa Serikali za Mitaa, wao vyama vya upinzani walikuwa wanahamasisha maandamano kwa wananchi na hivyo upinzani utaendelea kushindwa mbele ya CCM.
Akiwa katika Kata ya Buhoro (Kasulu Vijijini), Mhe. Vuma Holle amesema Tanzania imepiga hatua katika ujenzi wa Barabara za lami kutoka Kilomita 86,472 (Mwaka 2020) hadi Kilomita 91,532 (2023). Barabara za Changarawe Kilomita 893.04 (Mwaka 2020) hadi Kilomita 1042.43 (Mwaka 2023).
Aidha, Mbunge Vuma Holle amesema Hadi sasa jumla ya Vijiji 5,481 vimesambaziwa umeme na kufanya jumla ya vijiji 11,837 sawa na 96.37% kati ya Vijiji 12,318 vya Tanzania Bara.
"Kwa mambo mengi yaliyofanywa na Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania inayoongozwa na Rais, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan yanazidi kuweka imani kwa wananchi ya kuendelea kuipigia kura CCM na katika uchaguzi huu, CCM inaenda kushinda kwa kishindo nchi nzima" - Mhe. Augustine Vuma Holle, Mbunge wa Jimbo la Kasulu Vijijini
Attachments
-
WhatsApp Image 2024-11-25 at 09.32.33.jpeg184.7 KB · Views: 2 -
WhatsApp Image 2024-11-25 at 09.32.34.jpeg172.9 KB · Views: 3 -
WhatsApp Image 2024-11-25 at 09.32.34 (1).jpeg142.4 KB · Views: 2 -
WhatsApp Image 2024-11-25 at 09.32.35 (1).jpeg152.4 KB · Views: 2 -
WhatsApp Image 2024-11-25 at 09.32.36.jpeg114.6 KB · Views: 3 -
WhatsApp Image 2024-11-25 at 09.32.36 (1).jpeg105.7 KB · Views: 3 -
WhatsApp Image 2024-11-25 at 09.32.37.jpeg132.9 KB · Views: 2