Elections 2010 Mbunge wa Arusha apigwa hadi kuzirai na jeshi la polisi


Kaka au sijui ni dada tafadhali tuambie nini maana ya kupambana KISAYASI???? Hivi polisi anaruhusiwa kutoa hukumu kwa mtuhumiwa au ni mahakama? unamaanisha wale polisi walivyotoa ile adhabu kwa bwana Lema walitumia nguvu ya KISAYANSI SIO???
 

Lini wewe pia umekuwa ****?
 
Mimi nilikuwa natazama TV nikaona kipigo hiki cha Godbless Lema na Polisi walivyokuwa wanamchapa.

Inaonekana kwamba viongozi walioteuliwa na Serikali ya CCM wamesahau Katiba na Sheria ya Uchaguzi. Kilichotokea katika jimbo la Arusha Mjini ni kwamba wananchi wapiga kura walimchagua Godbless Lema kuwa Mbunge wao. Mbunge huyu amekwisha apizwa na ni Mbunge halali. Huyu ni MHESHIMIWA sasa na msamiati wetu unatambua hivyo.

Mbunge yeyote ana haki na uhuru kuhutubia waliompigia kura na kuwa na vikao na wananchi wa jimbo lake, kujadili nao jinsi ya kutatua matatizo yao. Polisi sio tu wamheshimu, bali wanatakiwa wampe ulinzi ili atekeleze wajibu na majukumu yake.

IGP Mwema anatakiwa atoe mwongozo kwa RPCs wote wazingatie kuwaheshimu Wabunge wa vyama vyote vya siasa. Polisi wakiheshimu Wabunge watakuwa wanaheshimu na kuenzi maamuzi ya wananchi. Polisi wa cheo chochote asiyeheshimu Mbunge, na hasa anayempiga au kumdhalilisha hafai. Afukuzwe.

Watumishi wa Serikali kama Mkurugenzi wa Manispaa wanatakiwa wakubali maamuzi ya wananchi wapiga kura. Kujaribu kuibeba CCM na kupindisha taratibu ili wawakilishi waliochaguliwa wasishiriki ni kubaka demokrasia na ni kinyume cha Katiba na sheria. Kuita Polisi katika mikutano ya madiwani, eti wawadhibiti ndio kuchochea fujo na kuweka vitisho visivyo na msingi. Madiwani wa vyama vyote vya siasa wawezeshwe kujadili na kushiriki katika vikao vyao, na ndivyo wananchi walivyotaka walipowachagua.
 
Nasubiri kusikia huyu bwana andengenya na yule mnali(aliyewacharaza mboko walimu) wanapandishwa vyeo,maana waapuz kama lema lazima wafundishwe adabu.

Mawazo yako ni finyu hata mtoto wa darasa la kwanza anakushinda, anyway, ni CCM ndio inakupa kiburi, lakini kumbuka machafuko yakitokea hayakuchagui. Hata wewe na uzao wako utaathirika.
 
"Mawazo yako ni finyu hata mtoto wa darasa la kwanza anakushinda, anyway, ni CCM ndio inakupa kiburi, lakini kumbuka machafuko yakitokea hayakuchagui. Hata wewe na uzao wako utaathirika."


jaribu kumwelewesha huyo asione walimu wamekaa kimya akadhani wamefurahi kwani me ni mwanafunzi wa shahada hiyo ya ualimu niliudhika sana. Halafu hii Tz yetu imekuwa kama nchi ya kusadikika wajumbe wema na wapenda maendeleo wamekuwa wakipigwa vta wakionekana ni wazushi. Me naanza kuamini wakina Shaaban Robert walikuwa wanaona mbali na ni manabii ambao hawakukubalika kwao.
 
Kwenye magazeti ya leo tunaona kauli za CCM zinavyojipinga zenyewe............................

Kwenye gazeti la majira lina kichwa cha habari Chadema watoa masharti ya mgogoro wa Mameya..........................

Uhuru lasema...................Makamba amjibu Lowassa.....................Asema CCM haitaongea na Chadema.....CCM isihusishwe na vurugu za Arusha.....wengi wamshangaa..................

The CItizen ..........Chadema tells Tendwa to call urgent meeting...............................

Daily News................CCM speaks on Arusha violence........defends Lowassa........................................

Yote haya yaashiria ya kuwa busara bado siyo sera ya CCM ila ni mabavu tu.........na hili haliisaidi taifa hata chembe..............................

Mtanzania.........................Makmba amrulka Lowassa..................................
 
watatiwa adabu mpaka wakome. wao si walisema asiyefunzwa na mamake afunzwe na ulimwengu? hiyo ndiyo habari
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…