Elections 2010 Mbunge wa Arusha apigwa hadi kuzirai na jeshi la polisi

Elections 2010 Mbunge wa Arusha apigwa hadi kuzirai na jeshi la polisi

Kila mtu ameshuhudia nini kilichotokea kwa Mheshimiwa Mbunge wa Arusha Mjini. Alinyanyuliwa kitini kwa nguvu na Polisi na kisha kupewa kipigo cha mbwa mwizi, haya yote yamefanyika LIVE kila mtu akiangalia. Hili halijafanyika kwa bahati mbaya, bali lilipangwa rasmi kwa hali ilivyokuwa ikijionyesha. Naomba kuuomba uongozi wa CDM umtake IGP Saidi Mwema atoe maelezo juu ya hali hiyo na pia wamtake amfukuze kazi huyo RPC, maana ni kinyume na sheria na utaratibu mzima wa kumchukulia hatua kiongozi yeyote aliyechaguliwa na wananchi.

Tunaweza kutofautiana kiitikadi za vyama..lakini nilichoshuhudia siku ile kweli kilinisikitisha. Mh. Lema ni kiongozi wa wananchi aliyechaguliwa kihalali, hivyo kumshushia kipigo kiasi kile sio tu kinaonyesha kutokuwa proffesional lakini nadhani wamesukumwa na hisia za kisiasa. Nadhani mambo kama haya ndio yanayopelekea uvunjaji wa amani. Pole kaka Lema kwa kipondo ulichokipata.
 
Well:

Ukiangalia ile "fracas" kati ya Lemma (MP) na Police Detectives utaona kuwa Lemma alikataa kutii "order" ya kumtaka asilete vurugu mahali pale (uhalali wa order is questionable though), halafu yeye in return akachomoa "pistol" (as self defence?) ndipo Police Detectives (seems kule Arusha kuna special forces wa kutosha) waka-hit the most sensitive parts/mishipa ya fahamu kujaribu kum-subdue in very quickest possible way!
 
Well:

Ukiangalia ile "fracas" kati ya Lemma (MP) na Police Detectives utaona kuwa Lemma alikataa kutii "order" ya kumtaka asilete vurugu mahali pale (uhalali wa order is questionable though), halafu yeye in return akachomoa "pistol" (as self defence?) ndipo Police Detectives (seems kule Arusha kuna special forces wa kutosha) waka-hit the most sensitive parts/mishipa ya fahamu kujaribu kum-subdue in
very quickest possible way
!

Hamna cha order wala nini. Ilipangwa iwe hivyo tena wangefurahi angekufa ati.
 
Binafsi nasikitika kuona baadhi yetu tunafurahia Lema kupigwa. Sijui waliompigia kura nao wangejibu mapigo ingekuwaje. Tumuombe Mungu atuepushe na balaa la ushabiki. Nyie askari mliompiga Lema mnaishi wapi? Hivi CCM mnafikiri mtawaongoza wa-TZ kwa nguvu zaidi? Mbona matatizo mengi yanakuwa kwenye maeneo ambayo CCM hawako vema? Sishabikii chama isipokuwa naipenda Tanzania yenye kujengwa na watanzania wasio na matabaka, udini, ukabila wala itikadi za kisiasa bali wenye uzalendo na nchi yao. Naomba tujiulize nguvu hizi zinazotumika kuuzima upinzani ni kwa faida ya nani? Au ukiwa CCM unakuwa mtanzania sana na ukiwa upinzania unakuwa sio mtanzania halisi?
 
Well:

Ukiangalia ile "fracas" kati ya Lemma (MP) na Police Detectives utaona kuwa Lemma alikataa kutii "order" ya kumtaka asilete vurugu mahali pale (uhalali wa order is questionable though), halafu yeye in return akachomoa "pistol" (as self defence?) ndipo Police Detectives (seems kule Arusha kuna special forces wa kutosha) waka-hit the most sensitive parts/mishipa ya fahamu kujaribu kum-subdue in very quickest possible way!

Ivi unacho kiongea unakijua au umetumwa wewe???
Unajua kuwa Mbunge ana Immunity yake hiyo mmoja??
Kwa kuangalia tuu ulidhania kuna fujo au hao police walitumwa kwani mikakati ilishakuwa imepangwa?
Tokea lini kwenye kikao kama hicho kina Police ndani?
Hivi uliuliza kwanini Kikao kilianza bila kuwa na idadi ya watu?

Je nani hapo aliashiria Fujo mwendesah uchaguzi au Lema nani alisababisha kuwepeo na mkanganyiko kama sio aliyekuwa anaendesha huo mkutano kwa kukiuka kanuni za huo mkutano

 
Mwisho wa ccm umefika hata wao hawaamini
ndiyo maana katiba mpya ni ya lazima na
hio ndio kaburi la ccm na ndio mwanga wa
maisha bora kwa masikini wa inchi hii
 
Kwa niliyoyasikia toka Arusha kwa mkereketwa wa CDM Mheshimiwa LEMA ALIOMBA KICHAPO KILE YEYE MWENYEWE!!
  1. Wao CDM walishagoma kwenda kwenye uchaguzi, wenzao wakaendelea! Kama sheria ilikiukwa (na CCM) basi CDM wangesubiri kupinga hilo kwa kufuata sheria!!
  2. Kuingia ukumbini wakati kikao cha uchaguzi (walichokigomea CDM) kimemalizika na kuanzisha vurugu ya kupinga matokeo ilitafsiriwa kama "kuvuruga amani"...na mbaya zaidi...
  3. Sheria ya nchi (Under the Criminal Procedures Act ikisomwa pamoja na Law of Evidence na Katiba yetu) inawaruhusu Polisi (au mtu yeyote aliyepewa dhamana ya kulinda usalama) kutumia "nguvu ya kiasi" wakati wa kumkamata (Arrest) na kumdhibiti (restrain) mhalifu/mtuhumiwa asilete madhara!! Bwana Lema alitoa BASTOLA, ni dhahiri endapo asingedhibitiwa angeweza kumdhuru mtu (Kwa kuwa kisheria huwezi kuelewa state of mind ya mtu wakati anafanya tendo lolote lile)....Kwa hiyo ilikuwa ni halali kwa polisi kumkamata na kumnyong'onyeza maana akkuwa anaendelea kutishia na hakujisalimisha kwa polisi!! Isitoshe polisi hawajatumia bastola au silaha nyingine, wametumia Judo na virungu...which so far was reasonable force!!
SOMO
Tunaipenda CDM lakini mbinu zake sasa zinatuchosha, watapigwa sana kama hawatakaa chini na kujadili mbinu mbadala! Wote tunajua kwa nini RPC Arusha alibadilishwa, yule jamaa na watu wake wako kwa kazi maalumu, wanasubiri kuwa "tuned" tu, sasa kama adui umeshamuelewa anakupaje kazi kupambana naye? Hebu CDM wafuate sheria, wapambane KISAYANSI siyo kwa kutumia nguvu "ZA KIJINGA"....Kamwe hatutaweza kushindana na dola....TUWE MAKINI
Watu tukiamua kuchapana na polisi kwa mbinu zetu hakuna watakaobaki. Yaani niliangalia what was being done kwa watu 15 kumshambulia armless person nikaona ni ujinga tu. We might turn this country in a civil war guy. Usidhani kuwaacha polisi ni kwamba wana uwezo kuliko sisi raia. NOoooooooooooo hatutaki tu kuifanya nchi ilindime wewe!. Mbinu za ugomvi ni nyingi. Tumejifunza judo na kung fu pia so, we acha tu......... Lakini siku tukikasirika polisi wetu hawa, hawa hawa ninaowafahamu, tukikasirika sisi wananchi, hawatakaa karibu kudadadeki.
 
Kila mtu ameshuhudia nini kilichotokea kwa Mheshimiwa Mbunge wa Arusha Mjini. Alinyanyuliwa kitini kwa nguvu na Polisi na kisha kupewa kipigo cha mbwa mwizi, haya yote yamefanyika LIVE kila mtu akiangalia. Hili halijafanyika kwa bahati mbaya, bali lilipangwa rasmi kwa hali ilivyokuwa ikijionyesha. Naomba kuuomba uongozi wa CDM umtake IGP Saidi Mwema atoe maelezo juu ya hali hiyo na pia wamtake amfukuze kazi huyo RPC, maana ni kinyume na sheria na utaratibu mzima wa kumchukulia hatua kiongozi yeyote aliyechaguliwa na wananchi.

we mbaba, kazi ya uteuzi bado haijaisha! labda mwambie igp ajiuzulu siyo kumwajibisha polisi aliyetetea ccm kikamilifu!!
 
Huu ni mwanzo tu, Mh. Mlema asubiri vipigo zaidi mama aliyemuangusha ubunge akiukwea ukuu wa mkoa
 
Kama alikuwa anabisha wafanyeje zaidi ya kipigo?tii amri uone mambo yanavyokwenda safiii
tatizo beki 3 akijua kushika keboard tabu sana...wewe unafikilia Lema ni kuku wa kisasa....acha ushabiki wa kijinga
 
tatizo la negative minded people. Mbona hamtaji sababu zilizopelekea kichapo cha LEMA???????????
CHADEMA Mnapenda kuvunja sheria kwa makusudi halafu mlalamike kuwa mnaonewa. Jeshi limefanya kazi yake. Naomba nipewe sababu za kichapo

MIMI NINAAMINI WEWE MUYA NDIO NEGATIVE MINDED PERSON WITH VERY LITTLE THINKING -TRY TO OPEN UP YOUR THINKING CAPACITY -AND THINK OUTSIDE THE BOX, TALK THE FACTS
1. ccm walizimisha mbunge wa viti maalum kupitia tanga apigie kura ccm eti kisa mwenyekiti mkoa arusha -hii ni kuvunja sheria au? jibu unalo
2. Mkurugenzi anatakiwa kuendesha kikao cha madiwani cha kuchagua meya na naibu wake baada ya idadi ya wajumbe kufika ukiondoa wajumbe yaani madiwani wa chadema 2/3 haipo nani kavunja sheria wewe muya????? jibu unalo
3. Hon. Lema aliwambia waliitisha kikao hicho wakati wametoa barua ya semina bila kuwajulisha chadema wapi kuna haki???
4. Police kazi yao ni kulinda amani raia na mali zake kwakuwa mheshimiwa Lema alikuwa anahoji utaratibu na ccm kwenda kumwita OCD amutoe Lema kwenye kikao na hivyo OCD kutumia Polisi hiyo ni haki? Tuambie wewe muya unajua sheria
5. Tangu uzaliwe ni lini ulisikia mbunge wa ccm kapigwa hata kofi na polisi zaidi ya mgombea mbunge wa shinyanga kumpiga mtama OCD kule Maswa je angekuwa Shibuda ndio kampiga OCD ingekuwaje?? hiii inasikitisha saana.
6. Kwa ujumla CCM sasa inaonesha waziwazi sura yake halisi ya sasa na kwa vyovyote vile inachochea hasira na vurugu ipo siku tutasema vinginevyo harafu wewe muya sijui utatwambia lini -kipofu mkubwa au fisadi mkubwa wewe.
7. Mapolisi wa namna hii ipo siku nguvu ya umma itawaangukia ndio watapata adabu na fundisho
8. Ninaamini IGP hana uwezo wa kufanya lolote kwa ccm kupigwa kwa lema ni agizo la serikali kupitia mkurugenzi arusha mjini aliyekuwa akitekeleza amri ya aliyemtea kuhakikisha kwa kumwaga damu au vingenevyo chadema haiongozi jiji -yana mwisho haya
 
Nasubiri kusikia huyu bwana andengenya na yule mnali(aliyewacharaza mboko walimu) wanapandishwa vyeo,maana waapuz kama lema lazima wafundishwe adabu.
 
Alafu kinachochukiza zaidi kabla hawajamburuza walimtekenya kidogo, hawa watu ni wabaya kiasi chake.

Kwa red mkuu una maana gani? au alistuliwa kidogo, nimejaribu kupiga msuli kuelewa maana halisi lkn naona nazidi kupotea tu....
 
Jamani usanii mwingine ni mbaya sana. Mkurugenzi wa jiji aliwatangazia madiwani wote wakiwamo wa CCM kwamba kuna semina baada ya kutokubaliana kuhusu mamluki kutoka Tanga lakini baadae CCM wao wakaitana baadae Chadema wakshangaa kuwa wako peke yao ktk semina, wakakimbilia Manispaa wakakuta CCM wenzao na yule wa TLP wameshafanya uchaguzi na kujipa umeya na kumpa wa TLP Unaibu

Hivi haya matokeo........nayo hayaruhusiwi kupingwa mahakamani?
 
Hivi haya matokeo........nayo hayaruhusiwi kupingwa mahakamani?
Nimatokeo ya rais pekee ndiyo hayapigwi mahakamani...lakini ya madiwani,wabunge,meya nk unawapigatu....
 
Arusha yapata meya wawili
• Aliyepewa unaibu Meya awageuka CCM

na Ramadhani Siwayombe, Arusha


amka2.gif
SAKATA la uchaguzi wa Meya wa Arusha mjini limeingia katika sura mpya baada ya mkurugenzi wa manispaa ya Arusha Estomii Chang'a kusema uchaguzi uliofanywa na kumshirikisha mbunge wa Viti Maalumu mkoa wa Tanga Mary Chatanda ulikuwa na baraka za Kaimu Katibu wa Bunge Eliakimu P. Mrema. Chang'a alitoa ufafanuzi huo kwa waandishi wa habari jana wakati akijibu maswali ya waandishi kuhusiana na utata uliojitokeza kuhusu uchaguzi huo ambapo ilipelekea vurugu baada ya kutangazwa meya bila madiwani wa CHADEMA kuwepo.
Katika vurugu hizo mbunge wa jimbo la Arusha mjini, Godbles Lema alikamatwa na polisi kwa kichapo na kuswekwa rumande kwa saa kadhaa kabla ya kuachiwa na kulazimika kukimbizwa hospitali baada ya kuishiwa nguvu.
Akiongelea matukio hayo Mkurugenzi huyo alisema kufuatia utata uliojitokeza wa uhalali wa Mary Chatanda kupiga kura manispaa ya Arusha badala ya Tanga, alilazimika kuwasiliana na ofisi ya bunge kupata ufafanuzi ndipo alipoletewa barua iliyosainiwa na Mrema ikimhalalisha Chatanda kushiriki uchaguzi huo.
Alifafanua licha ya kupata ufafanuzi huo siku ya Ijumaa alilazimika kuahirisha kikao hicho cha baraza na kufanya kikao cha siri cha ndani siku ya Jumamosi ambapo madiwani wa CHADEMA hawakuhudhuria ndipo akalazimika kuendelea na taratibu za uchaguzi na kumtangaza Gaudensi Limo kuwa meya huku Michael Kivuyo akimtangaza kuwa ndie naibu meya.
Wakati mkurugenzi akitoa ufafanuzi huo aliyetangazwa kuwa Naibu Meya Michael Kivuyo (TLP) ameongea na waandishi wa habari jana na kusema uchaguzi uliofanyika haukuwa halali kwa kuwa ulikiuka baadhi ya kanuni za halmashauri.
Kivuyo alisema licha ya yeye kuchaguliwa kuwa naibu meya lakini atashirikiana na madiwani wa CHADEMA kupinga uchaguzi huo kwani ulikiuka taratibu mbalimbali za kikanuni za halmashauri.
Alipoulizwa kuhusu wadhifa wake kama ataendelea kuwa nao wakati anapinga uchaguzi huo alisema anawasiliana na chama chake ili atoe tamko la kujiuzulu nafasi hiyo ya unaibu meya kwa kuwa uchaguzi uliomchagua haukuwa halali.
Wakati hayo yakiendelea, madiwani wa CHADEMA hadi jana jioni walikuwa wanaendelea na kikao cha kumchagua meya wa jiji la Arusha ambapo nafasi hiyo ilikuwa ikiwaniwa na diwani wa kata ya Kimandolu Estomii Mala.
Akiongea na Tanzania Daima msemaji wa madiwani wa CHADEMA John Bayo alisema kuwa wao wanachagua meya wao na leo watamsindikiza katika ofisi za manispaa ya Arusha kuanza kazi za umeya.
Hali hiyo inamaanisha kuwa kutakuwa na mameya wawili katika ofisi moja hali ambayo si ya kawaida kutokea katika historia ya siasa za nchi hii.
Kwa hali hiyo, kinachotokea Arusha katika ngazi ya umeya kinafafana kabisa na kile kilichojitokeza nchini Ivory Coast ambapo nchi hiyo sasa inaongozwa na marais wawili baada ya kila moja kujitangaza rais.
Uchaguzi huo wa kumpata Meya wa jiji la Arusha uliingia tafrani kutokana na vyama vya CCM na CHADEMA kulumbana katika masuala ya kanuni, CHADEMA wakipinga mbunge wa viti maalum Mary Chatanda (CCM) kuwa mjumbe wa mkutano huo huku CCM nao wakipinga mbunge wa viti maalumu wa Rebecca Mgondo (CHADEMA) kuwa hajaapishwa kuwa mbunge hivyo hastahili kuwa mjumbe wa kikao hicho.
Wakati yote hayo yakiendelea, aliyetangazwa kuwa meya wa jiji la Arusha Gaudensi Lyimo (CCM), jana aliitisha kikao na waandishi wa habari chini ya ulinzi wa maofisa kadhaa wa polisi waliovalia kiraia, kuzungumzia yaliyojitokeza katika uchaguzi.
Kitendo hicho kiliwakera waandishi wa habari na kulazimika kumhoji Lyimo kwa kumtaka aeleze sababu za kuwaita askari kanzu hao katika kikao chake hicho kinyume na taratibu za kawaida za vikao kama hivyo vya wanahabari.
Katika majibu yake, Lyimo alijitetea kuwa wana usalama hao wamelazimika kuwepo kwa ajili ya kuangalia usalama wa eneo hilo kutokana na hali inayoendelea hivi sasa tangu kuvurugika kwa mkutano wa baraza la madiwani ambao yeye alitangazwa kuwa meya wa Arusha.
Majibu hayo hayakuweza kukidhi haja ya waandishi wa habari na kufikia hatua ya kulaumu halmashauri hiyo ya manispaa ya Arusha kuanza kutumia vyombo vya dola vibaya kitendo ambacho hata siku ya kikao cha baraza vilitumika kuwasambaza wananchi waliofika kutaka kusikiliza kikao hicho cha kwanza na kurushiwa mabomu ya machozi.
"Tunaomba tukwambie wazi kuwa kama ndio staili hii umeingia nayo, ofisini hii tutakuwa hatuji katika mikutano yako hata kama umetualika. Kutuletea askari ni kuingilia uhuru wa habari kwani tutakuwa tunashindwa hata kuuliza baadhi ya maswali kutokana na kukaa kwa hofu," alisema Moses Mshala mwandishi wa habari wa gazeti la Mwananchi.
Aidha, akizungumzia suala hilo mwandishi wa habari wa gazeti la Raia Mwema, Paulo Sarwat, alisema kitendo cha polisi kuwafukuza waandishi katika kikao hicho cha baraza la madiwani ni cha udhalilishaji mkubwa kwa wanahabari na hali hiyo ikiendelea kuna hatari ya haki nyingi za wananchi kuhodhiwa bila maelezo ya msingi.
Baada ya malalamiko hayo ya waandishi dhidi ya udhalilishaji huo, ofisi ya mkurugenzi ililazimika kuomba radhi kwa kilichotokea na kuahidi hakitajirudia tena katika siku zijazo.
 
Umeya Arusha utata mtupu Send to a friend Monday, 20 December 2010 20:27 0diggsdigg

Moses Mashalla, Arusha
UTATA wa uchaguzi wa umeya jijini Arusha umechukua sura mpya mara baada ya naibu meya aliyechaguliwa juzi ambaye pia ni diwani wa TLP katika kata ya Sokoni jijini Arusha, Michael Kivuyo kuibuka na kutoa matamko mawili tofauti moja likiwa ni kutoutambua uchaguzi uliofanyika kwasababu ulikuwa ni batili jingine ni kukubali uteuzi wa nafasi yake katika uchaguzi huo.

Hatahivyo nao uongozi wa Manispaa ya Arusha chini ya msimamizi wake,Estomi Chang'a pamoja na ofisi za meya wa nayo kwa pamoja jana waliibuka na kutoa ufafanuzi juu ya utata uliojitokeza katika uchaguzi huo
Tamko hilo la naibu meya huo lilionekana kuzua kizazaa jijini hapa ambapo alilitoa katika hoteli ya Equitor iliyopo mkabala na ofisi za manispaa wakati akihojiwa na waandishi wa habari waliotaka kujua msimamo wake kwa sasa baada ya uteuzi huo.

Akizungumza na waandishi wa habari majira ya saa 7;30 mchana, naibu meya huyo aliasema uchaguzi uliofanyika ni batili kwa sababu idadi ya theluthi mbili za wajumbe waliopaswa kupiga kura haikutimia na hivyo kuuita kuwa ni batili.
Mbali na sababu hiyo, Kivuyo alipigilia msumari akisisitiza kitendo cha mbunge wa viti maalumu mkoani Tanga, Mary Chatanda kupewa ruhusa ya kupiga kura kilikuwa na uwalakini kutokana na yeye kutokuwa mwakilishi wa Mkoa wa Arusha.

"Msimamo wangu uko wazi kabisa uchaguzi ulikuwa batili kwani column (idadi) ya wajumbe haikutimia, lakini kitendo cha kumruhusu mbunge wa viti maalumu Mkoa wa Tanga kupiga kura nacho hakifai na nilishasema kabisa hata ITV"alisema Kivuyo.

Wakati huo huo katika mkutano ulioitishwa jana na meya wa Manispaa ya Arusha, Gaudence Lyimo, naibu meya huyo alipoulizwa na waandishi wa habari juu ya madai ya yeye kutoutambua uchaguzi huo ihali ndio uliomuingiza madarakani, Kivuyo alishikwa na kigugumizi na kudai mbali na kutoutambua, lakini anakubali uteuzi wa nafasi yake.
"Lakini mimi nakubali kuwa ni naibu meya"alisema Kivuyo kabla ya kuomba ridhaa ya kuondoka katika kikao na wanahabari.

Katika mkutano wa ufafanuzi juu ya utata uliofanyika ndani ya ofisi za meya mkurugenzi wa manispaa hiyo, Chang'a alifafanua utata wa suala la Chatanda na kwamba mwakilishi huyo aliruhusiwa kupiga kura kutokana na maagizo kupitia kwa ofisi ya Bunge la Jamhuri la Tanzania.
Chang'a alisema mara Chadema walipoibua hoja ya Chatanda ilibidi awasiliane na Ofisi ya bunge na kupatiwa maagizo ya barua iliyotumwa kwa nukushi yenye KUMB,NA CEB.77/77/155/01/79 ya desemba 17 iliyosaniwa na Naibu Katibu wa Bunge, Eliakimu Mrema ambapo barua hiyo ilimtambua Chatanda kama mjumbe halali wa Manispaa ya Arusha.
"Mara baada ya hoja ya Chatanda kuibuliwa na Chadema ilibidi nipate ufafanuzi kupitia ofisi ya bunge ambapo walituma barua kwa fax kuwa Chatanda ni mjumbe halali wa manispaa ya Arusha"alisema Chang'a

Kuhusiana na suala la idadi ya wajumbe kutotimia ili kuweza kumchagua meya na naibu wake, mkurugenzi huyo alifafanua kwamba suala hilo sio kweli kwani nusu ya wajumbe ambao ilikuwa ni madiwani 17 walitosha kupiga kura katika uchaguzi huo kwa taratibu za kisheria.

"Hili suala la Chadema kudai kuwa idadi ya theluthi mbili ndio wanapaswa kufanya uchaguzi halipo mimi nilipoona wajumbe 17 wanatosha kufanya uchaguzi nikaamua kuitisha sasa utata uko wapi"alifafanua Chang'a
 
Kila kitu kuchakachua tu......Huyu Meya si halali na hataweza kutawala kwa mujibu wa sheria......Haiingii akilini kabisa meya achaguliwe kinyume cha sheria alafu akubaliwe! Katu hakipo kitu kama hicho lazima swala lipelekwe mahakamani ili huyu mtu ashughulikiwe maana sasa watanzania tumechoka kubururwa na demokrasia ya ajabu hii....
 
Back
Top Bottom