Shkh Yahya
Senior Member
- Oct 1, 2010
- 100
- 5
Kila mtu ameshuhudia nini kilichotokea kwa Mheshimiwa Mbunge wa Arusha Mjini. Alinyanyuliwa kitini kwa nguvu na Polisi na kisha kupewa kipigo cha mbwa mwizi, haya yote yamefanyika LIVE kila mtu akiangalia. Hili halijafanyika kwa bahati mbaya, bali lilipangwa rasmi kwa hali ilivyokuwa ikijionyesha. Naomba kuuomba uongozi wa CDM umtake IGP Saidi Mwema atoe maelezo juu ya hali hiyo na pia wamtake amfukuze kazi huyo RPC, maana ni kinyume na sheria na utaratibu mzima wa kumchukulia hatua kiongozi yeyote aliyechaguliwa na wananchi.
Tunaweza kutofautiana kiitikadi za vyama..lakini nilichoshuhudia siku ile kweli kilinisikitisha. Mh. Lema ni kiongozi wa wananchi aliyechaguliwa kihalali, hivyo kumshushia kipigo kiasi kile sio tu kinaonyesha kutokuwa proffesional lakini nadhani wamesukumwa na hisia za kisiasa. Nadhani mambo kama haya ndio yanayopelekea uvunjaji wa amani. Pole kaka Lema kwa kipondo ulichokipata.