Mbunge wa Bagamoyo: Serikali isisikilize maneno uuzaji wa akiba ya dhahabu, Wanaharakati uchwara wapuuzwe

Mbunge wa Bagamoyo: Serikali isisikilize maneno uuzaji wa akiba ya dhahabu, Wanaharakati uchwara wapuuzwe

Waufukweni

JF-Expert Member
Joined
May 16, 2024
Posts
5,383
Reaction score
18,776
Mbunge wa Bagamoyo (CCM), Subira Mgalu, ameishauri Serikali kutoyumbishwa na maoni ya wanaharakati na wakosoaji kuhusu mpango wa kuuza sehemu ya akiba ya dhahabu ya Taifa kwa ajili ya kugharamia miradi ya kimkakati.

Akichangia mjadala wa hotuba ya Rais bungeni jijini Dodoma leo, Januari 30, 2026, Subira amesema uamuzi huo ni wa kizalendo na unalenga kupunguza utegemezi wa mikopo ya nje kwa kutumia rasilimali za ndani.

Subira amekumbusha kuwa ni katika uongozi wa Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan ambapo historia iliandikwa kwa Benki Kuu ya Tanzania (BoT) kuanza kununua na kuhifadhi dhahabu, hatua ambayo imewezesha nchi kukusanya zaidi ya tani 1.7 na kuingia kwenye orodha ya mataifa 10 bora Afrika yenye akiba kubwa ya madini hayo.

Soma: Tanzania yapanga kuuza sehemu ya Hazina yake ya Dhahabu kusaidia kufadhili miradi ya miundombinu

Mbunge huyo amewataka Watanzania kutokuwa na taharuki, akieleza kuwa uuzaji wa akiba hiyo ni uamuzi wa kitaalamu na wa kimkakati uliolenga kuhakikisha miradi mikubwa ya nchi haikwami

“Uamuzi wa Serikali wa kununua dhahabu ulikuwa wa kihistoria. Leo Serikali inafanya maamuzi ya kuuza sehemu ya akiba yake kwa ajili ya kugharamia miradi ya kimkakati. Naunga mkono hatua hiyo na naomba Serikali isisikilize maneno ya watu ambao hawaitakii mema Taifa letu. Kimfaacho mtu chake,” amesema Subira.

 
Kwanini tusibane matumizi ili kufadhili miradi? Mfano kupunguza masafari, ukubwa wa serikali, kuondoa vyeo vinavyo overlap kama DC, DED, DAS, Mayor akabaki mmoja tu!!

Mambo kama Mwenge, sijui goli la mama, viti maalum, na hizo unnecessary costs mbona tutasave pesa za kutosha tu.

Ila kuuza akiba wakati hatujui ya kesho ni maamuzi mabovu kabisa. Zaidi fedha za miradi zitaishia mifuko ya mafisadi huku tayari dhahabu zimeenda!!
 
Ila alikuwa amejtahidi kutunga shahiri ila ameshindwa kuzingatia ulali wa vina na mizani
 
Sasa uyu GenZ wakimchomea nyumba yake moto, au gari yake kutakuwa na kosa gani kwa Genz wambieni wabunge nchi bado imevimba sasa wao kujichetua akili na kuongea mambo ya ajabu ajabu watu wanawaskia haya
 
Back
Top Bottom