PreGE2025 Mbunge wa Buchosa Eric Shigongo ameanza rasmi Kampeni ya `Buchosa inaongea katika Kata ya Nyehunge

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla)

Richer

JF-Expert Member
Joined
Jun 9, 2025
Posts
2,318
Reaction score
4,079
Mbunge wa Buchosa, Eric Shigongo, ameanza rasmi kampeni ya kufungua barabara za mitaa kwa mtindo wa kitongoji kwa kitongoji, ikiwa ni sehemu ya jitihada za kuboresha miundombinu na kurahisisha usafiri kwa wananchi wa Buchosa

Zoezi hilo limeanza katika Kata ya Nyehunge, likitekelezwa na mitambo maalum aliyoinunua mwenyewe kwa ajili ya kuisaidia serikali kuwahudumia wananchi.

Kampeni hiyo inayofahamika kwa jina la 'Buchosa Inaongea' inalenga kufungua barabara katika kata zote 21 na vijiji vyote 82 vya jimbo hilo

Mbunge Shigongo amesema ataendelea kutumia nguvu zake zote kuwatumikia wananchi ili kuhakikisha wanafaidika moja kwa moja na huduma za serikali yao

huyu hashindi,tizeba anarudi
 
Yani ndio aanze leo? Wana Buchosa wanatakiwa wamkimbize kama wameona panya ndani.​
 
Back
Top Bottom