Mbunge wa CCM ahoji walimu wakuu kusimamia ujenzi wa madarasa na nyumba za walimu

Mbunge wa CCM ahoji walimu wakuu kusimamia ujenzi wa madarasa na nyumba za walimu

peno hasegawa

JF-Expert Member
Joined
Feb 24, 2016
Posts
18,223
Reaction score
31,465
Dodoma. Mbunge wa viti maalum (CCM), Munde Tambwe ameitaka Serikali kuachana na utaratibu wa walimu wakuu kupewa kazi ya kusimamia ujenzi katika shule zao kwa kuwa si wataalamu wa mambo ya ujenzi na uhasibu.

Munde ameyasema hayo leo Alhamisi Juni 16, 2022 wakati akichangia mjadala wa bajeti kuu ya Serikali kwa mwaka 2022/23.

“Tumekuwa tukifanya mambo ya ajabu, fedha zinakwenda kwenye shule kujenga madarasa na kadhalika, anaambiwa mwalimu mkuu asimamie majengo. Mwalimu mkuu ana utaalamu gani wa kusimamia majengo," amehoji.

Amesema walimu hao hawajasomea uhasibu lakini wanakwenda kukaguliwa na kwamba shule ina walimu wachache lakini anatolewa mwalimu mkuu kwenda kusimamia ujenzi wakati wamekuwa wakilalamikia kuwa idadi yao haitoshi nchini.

“Niiombe Serikali itafute wataalam wa kufanya hiyo kazi na walimu waachwe wafanye kazi zao za elimu. Wamekuwa wakilaumiwa sana katika hili. Kwa mfano jengo la nyumba ya mwalimu linajengwa kilometa moja kutoka shuleni nani anampa hiyo nauli ya kwenda kusimamia jengo hilo,” amesema.

Aliitaka Serikali kutowakamata walimu hao inapotokea kasoro katika ujenzi kwa sababu si wahandisi wa kuweza kusimamia ujenzi wa majengo hayo.
 
Walimu kusimamia miradi , ile ilikuwa sera ya kijinga ya mwendazake.

Ati hiyo ndo Force Account.

Ni sera inayowapeleka walimu wengi lupango wakati huku nyuma inaliwa na watendaji wa Halmashauri.

Prof Mkenda anashindwa kujibu kwa vile anaelewa ila anaogopa kujibu.
 
Hivi sheria ya Manunuzi inaruhusu Mwalimu asiye weledi au utaalamu unaorasimishwa na PSPTB kufanya manunuzi? Na wakirogwa kuwafikisha mahakamani wanabwagwa kirahisi. Hapo kuna uchezewaji wa taaluma za watu
 
Of course huu ni ujinga na utoto..

Halmashauri zina vitengo vya miundombinu na kama haitoshi kuna TBA ambae anaitwa wakali wa majengo sasa sijui majengo gani wanasimamia..
 
Wakati mwingine kama hulielewi jambo..rudia mara na mara kufikiri, hivi yale majengo ya zahanati, madarasa ya shule nk ambayo wanakijiji huwa wanajenga kwa kujitolea nani huwa anajenga? Ni mkandarasi? Nyumba za watu vijijini nani huwa anajenga? Usimamizi wa jambo lolote ni taaluma ya kusomea?

Muundo wa usimamizi wa shule zetu, zahanati, vituo vya afya nk unaongozwa na kamati za mahali ambazo hujumuisha watu mashuhuri kwenye kijiji kile, wataalam nk..hao wote hawawezi kusimamia majengo mawili au matatu ya kujenga? au tanki la maji la kijiji..km huwezi kuona uhalisia wa style hii ya usimamizi wa shughuli za ujenzi, basi pengine kichwani hakuko sawa una mapungufu.

Hata hivyo lengo ni kuleta sense ya watu wa eneo hilo kufeel ile hali ya kuwa kitu hiki ni Chao na hivyo wakijenge vzr wakitunze kidumu..lkn pia kuleta multipler effect ya miradi kwa watu wa kijijini..sasa ubaya uko wapi, wizi ni hulka ya mtu kama tu ambavyo si wakandarasi wote ni wezi.
 
Halafu wanakamatwa na kupata misukosuko wakikosea. For sure it is not fair.
 
Walimu kusimamia miradi , ile ilikuwa sera ya kijinga ya mwendazake.
Ati hiyo ndo Force Account.
Ni sera inayowapeleka walimu wengi lupango wakati huku nyuma inaliwa na watendaji wa Halmashauri.

Prof Mkenda anashindwa kujibu kwa vile anaelewa ila anaogopa kujibu.
Sera kama haikuwa rafiki si wangeitoa! Kwani aliwaambia mkiitoa ni laana? Mnajazia chuki tu, aligoma ye kusafiri mkaingia mkaona ni ujinga ni safari kwenda mbele, iweje hizi sera ndo mlaumu wakati hela hakuzileta yeye na maamzi mlikuwa nayo ninyi?
 
Back
Top Bottom