PreGE2025 Mbunge wa CCM aipinga bajeti ya ujenzi, awaita mawaziri waongo

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla)

Mkalukungone Mwamba

JF-Expert Member
Joined
Aug 29, 2022
Posts
3,141
Reaction score
7,205
Mbunge wa Sumve (CCM), Kasalali Mageni leo Jumanne Mei 6, 2025 amekuwa mbunge wa kwanza kusikika akipinga bajeti ya Serikali kwa madai ya kuchoshwa na uongo.

Mageni ameipinga bajeti ya Wizara ya Ujenzi iliyowasilishwa jana Jumatatu, Mei 5, 2025 na Waziri wa Ujenzi, Abdallah Ulega ambaye aliomba Bunge limpitishie Sh2.28 trilioni kwa ajili ya miradi ya maendeleo na matumizi mengine.

Kauli ya Mageni inakuwa ya kwanza kusikika tangu mkutano wa 19 katika Bunge la 12 maalumu la kujadili bajeti za Serikali jijini Dodoma tangu ulipoanza Aprili 8, 2025 ambapo wabunge wamekuwa wakiunga mkono tangu kuanzia hotuba ya Waziri Mkuu na zilizofuata.

Kupata matukio na taarifa zote kwa kila mkoa kuelekea Uchaguzi Mkuu 2025 ingia hapa: Special Thread: Mijadala na Matukio ya Uchaguzi Mikoa yote Tanzania Bara na Zanzibar kuelekea Uchaguzi Mkuu 2025

Amewataja marais watatu, Benjamin Mkapa, Jakaya Kikwete, John Magufuli ambao kwa nyakati tofauti walipofika wilayani humo, Mkoa wa Mwanza waliahidi ujenzi wa barabara lakini hilo halikufanyika na wilaya hiyo imeendelea kutounganishwa kwa lami.

Ameshachelewa amekumbuka shuka kumeshakucha hata sisi wananchi hutumungi mkono mbunge
 
Hayo alitakiwa azungumze na wananchi wake toka mwanzo wa ubunge wake. Sasa anakwenda kulialia Bungeni atapata faida gani; wakati akijuwa wazi jina lake litakatwa mapema kabisa kwenye mchujo unaofuata!
 
Shida sio yeye aliahidiwa
 
Shida sio yeye aliahidiwa
Nani aliahidiwa, wananchi? Kama ni wananchi waliahidiwa na kutotimiziwa hiyo ahadi; bado ni swala la mbunge kuwakumbushia wananchi mara kwa mara kuhusu ahadi hiyo ambayo haijatimizwa. Ikwa hivyo, mbunge hawezi kuwa na lawama yoyote kwa wananchi, na hata hofu ya kukatwa jina isingekuwepo.
 
Usipende kuona watu wengine hawajui wanachokifanyaa yaani upo kama mtoto mlalamikaji tu nahujui baba yako anapitia nini sio kila mbunge amekuja kimaslahi wengine wanahangaika hawajui cha kufanya
 
Duh!

Yamekuwa haya tena. Mbona wala simlaumu mbunge; kwani sijui alichofanya huko jimboni kwake. Mimi natoa mawazo yangu tu kueleza ambacho kingetokea kama angesimamia uwakilishaji wake ipasavyo; pengine inawezekana kabisa alifanya hivyo, kwa hiyo hana sababu ya kuwa na hofu juu ya wananchi wake kutomuunga mkono.

Kwa vile wewe unamfahamu vizuri huyo mbunge na uwakilishi wake huko jimboni, kwa nini usieleze tu kwa kifupi; badala ya kuanza kulalamika kwa hofu tu kwamba anasemwa vibaya.
Tueleze, huko Bungeni aliwahi kulishikia sana bango swala hili huko siku za nyuma?
 
sio kila mbunge amekuja kimaslahi wengine wanahangaika hawajui cha kufanya
Mkuu 'SweetyCandy', sijasema popote kuwa huyu mheshimiwa hajafanya chochote, sijui kwa nini umechukulia maoni yangu kuwa lawama kwake.
Ninakubaliana na wewe moja kwa moja; ndani ya CCM sasa hivi wabunge wanaosifika siyo wale wanaopigania maslahi ya wananchi. Wabunge kama Kibajaji (Lusinde); akina Kashetu/sijui Kasheku, yule anayejiita "Msukuma". Hao ndio wabunge wenye maana kwa CCM ya siku hizi.
 
Back
Top Bottom