Mkalukungone Mwamba
JF-Expert Member
- Aug 29, 2022
- 3,141
- 7,205
Ameshachelewa amekumbuka shuka kumeshakucha hata sisi wananchi hutumungi mkono mbungeMbunge wa Sumve (CCM), Kasalali Mageni leo Jumanne Mei 6, 2025 amekuwa mbunge wa kwanza kusikika akipinga bajeti ya Serikali kwa madai ya kuchoshwa na uongo.
Mageni ameipinga bajeti ya Wizara ya Ujenzi iliyowasilishwa jana Jumatatu, Mei 5, 2025 na Waziri wa Ujenzi, Abdallah Ulega ambaye aliomba Bunge limpitishie Sh2.28 trilioni kwa ajili ya miradi ya maendeleo na matumizi mengine.
Kauli ya Mageni inakuwa ya kwanza kusikika tangu mkutano wa 19 katika Bunge la 12 maalumu la kujadili bajeti za Serikali jijini Dodoma tangu ulipoanza Aprili 8, 2025 ambapo wabunge wamekuwa wakiunga mkono tangu kuanzia hotuba ya Waziri Mkuu na zilizofuata.
Kupata matukio na taarifa zote kwa kila mkoa kuelekea Uchaguzi Mkuu 2025 ingia hapa: Special Thread: Mijadala na Matukio ya Uchaguzi Mikoa yote Tanzania Bara na Zanzibar kuelekea Uchaguzi Mkuu 2025
Amewataja marais watatu, Benjamin Mkapa, Jakaya Kikwete, John Magufuli ambao kwa nyakati tofauti walipofika wilayani humo, Mkoa wa Mwanza waliahidi ujenzi wa barabara lakini hilo halikufanyika na wilaya hiyo imeendelea kutounganishwa kwa lami.
Shida sio yeye aliahidiwaHayo alitakiwa azungumze na wananchi wake toka mwanzo wa ubunge wake. Sasa anakwenda kulialia Bungeni atapata faida gani; wakati akijuwa wazi jina lake litakatwa mapema kabisa kwenye mchujo unaofuata!
Nani aliahidiwa, wananchi? Kama ni wananchi waliahidiwa na kutotimiziwa hiyo ahadi; bado ni swala la mbunge kuwakumbushia wananchi mara kwa mara kuhusu ahadi hiyo ambayo haijatimizwa. Ikwa hivyo, mbunge hawezi kuwa na lawama yoyote kwa wananchi, na hata hofu ya kukatwa jina isingekuwepo.Shida sio yeye aliahidiwa
Usipende kuona watu wengine hawajui wanachokifanyaa yaani upo kama mtoto mlalamikaji tu nahujui baba yako anapitia nini sio kila mbunge amekuja kimaslahi wengine wanahangaika hawajui cha kufanyaNani aliahidiwa, wananchi? Kama ni wananchi waliahidiwa na kutotimiziwa hiyo ahadi; bado ni swala la mbunge kuwakumbushia wananchi mara kwa mara kuhusu ahadi hiyo ambayo haijatimizwa. Ikwa hivyo, mbunge hawezi kuwa na lawama yoyote kwa wananchi, na hata hofu ya kukatwa jina isingekuwepo.
Duh!Usipende kuona watu wengine hawajui wanachokifanyaa yaani upo kama mtoto mlalamikaji tu nahujui baba yako anapitia nini sio kila mbunge amekuja kimaslahi wengine wanahangaika hawajui cha kufanya
Mkuu 'SweetyCandy', sijasema popote kuwa huyu mheshimiwa hajafanya chochote, sijui kwa nini umechukulia maoni yangu kuwa lawama kwake.sio kila mbunge amekuja kimaslahi wengine wanahangaika hawajui cha kufanya